Ametoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Septemba 30, 2016) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Julai 25 kuwa atahamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.
“Tukio hili la kuhamia Dodoma si la mzaha, hakuna siasa na wala si jaribio. Tumeshakeleza. Kama kuna waliokuwa wanafiria kwamba halitekelezeki watambua kwamba tayari tumeshafika. Na kuanzia sasa atakayetaka huduma ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu amesema Dodoma si ndogo kama baadhi ya watu wanavyodai na kwamba huduma zilizopo zinatosha kukidhi mahitaji ya sasa. "Mkakati uliopo wa kupanua huduma za tiba, maji, umeme na masoko utawezesha watumishi wote kuishi bila bugudha yoyote."
“Awamu ya kwanza inaanzia Septemba hadi Februari mwakani. Mimi nimeshatangulia na wanaofuata ni mawaziri na manaibu wao wote, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wote. Natambua kwamba wote wana nyumba za kuishi na kama wapo ambao hawana hawazidi asilimia tano na nyumba zipo
Amewataka watumishi wote wa Serikali watambue kwamba safari imeshaanza na kila mmoja ajipange, na akarudia wito wa Mheshimiwa Rais kwamba atakayegoma kuhamia Dodoma atakuwa amejifukuza kazi.
Waziri Mkuu amewataka watendaji wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) wasifanye kazi kwa mazoea, bali wabadilike na kwa kuwa amehamia Dodoma ameahidi kuafuatilia kwa karibu zaidi.
Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi (OWM SUBKAV), Jenista Mhagama amesema kilichofanyika leo ni uthibitisho kuwa yale ambayo Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi sasa hivi imeanza kuyatekeleza.
"Tuliahidi kukusanya kodi, tuliahidi elimu bure, tuliahidi kupambana na mafisadi, tuliahidi kuondoa watumishi hewa, tuliahidi kuifufua ATCL na kununua ndege mpya na yote tumetekeleza,” amesema.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. George Simbachawene amesema uamuzi wa kuhamia Dodoma ni uthibitisho kuwa viongozi wetu kweli wamedhamiria kutekeleza ahadi ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu ya nchi hapa Dodoma.
"Dodoma imeanza kuchangamka na hii ni fursa tosha kwa mkoa wetu kubadilika. Tushirikiane na CDA kuijenga Dodoma mpya. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri Mkuu kuingia Dodoma leo hii maana yake ni kwamba Serikali iko rasmi Dodoma," amesema.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Manaibu Waziri Anthony Mavunde na Dk. Ashatu Kijaji, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais (Utumishi), Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo, wazee wa mkoa huo, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi zilizoko mkoani na baadhi ya wananchi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment