Mawali yapo gazeti la Mwananchi ukurasa wa mbele na amehojiwa Clouds Fm
1. Kwanini Makonda hukuchukua hatua dhidi ya hao watu 10 wanaomueleza wanataka kumpa 50Million Kila Mwezi ili kumyamazisha?
2.Kwanini hakutaja majina yao kwa Vyombo husika ili vifanye uchunguzi na Kuchukua hatua?
3. Alipoambiwa kuwa waziri mkuu karuhusu Shisha kwanini hakwenda kumuuliza hadi akayasema hadharani?
4. Kamanda Siro na Kaganda ni wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kwanini hakuwapa maelekezo huko na kwenda kuwachongea kwa waziri mkuu?
5. Hayo yote yanaibua Swali la Mwisho Kulikua na Ulazima gani wa kutoa tuhuma hadharani kwa viongozi hao wakati serikali Ina mfumo wake wa mawasiliano na vyombo ya Uchunguzi?
Majibu
Makonda amesema waandishi wahangaike kuelimisha kuhusu madhara ya shisha na sio kuhangaika na kauli ambayo haina madhara
Pia amesema kutamka hadharani ni kuongeza awareness
Pia amesema hakutaja majina kwa kuwa majina hayatajwi hadharani
Maana ya kumuuliza waziri mkuu hadharani ni ili umma upate majibu, akiuliza kwa kificho wengine wanaweza wasiamini majibu au wasiyapate
Makonda amedai ameshuhudia shisha inauzwa maeneo hadharani kabisa na kuuliza polisi wanasema hakuna
Makonda amesema wanafanya kazi kwa uwazi kwa hiyo hakuna haja ya kuficha ficha na kuulizana sirini
SIKILIZA HAPA:
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment