Nov 7, 2016

Mkataba wa EPA pasua kichwa....Wabunge Kuamua Hatima Yake

MKATABA wa Uhusiano wa Uchumi na Biashara Kati ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Ulaya (EPA), umegeuka kaa la moto baada ya mtalaamu wa sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Palamagamba Kabudi, kuainisha vifungu visivyofaa vinavyoweza kuiumiza nchi kama itaukubali.

Kutokana na hali hiyo wabunge wameitaka Serikali isiingie kwa haraka kwenye mkataba huo kwa kuwa hauna maslahi kwa Taifa.

Mkataba huo ambao hadi sasa  Tanzania haijausaini, unatarajiwa kuwasilishwa bungeni Alhamisi wiki hii kwa ajili ya kujadiliwa ingawa Kenya na Rwanda zimekwisha kuusaini.

Akiuchambua mkataba huo    kwenye semina ya wabunge mjini hapa jana, Profesa Kabudi, alisema mkataba huo haifai kwa kuwa una ahadi nyingi zisizotekelezwa.

Kwa mujibu wa mkataba huo, Profesa Kabudi alisema nchi za Ulaya hazitapata hasara yoyote ila nchi za EAC ndiyo itaathirika kwa sababu  hazitaruhusiwa tena kuongeza ushuru wa bidhaa zinazoingia katika nchi husika.

“EPA itasababisha wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kukosa ajira kutokana na ukanda huo kugeuka ukanda huru wa bidhaa za Ulaya.

“Kama tutausaini kisha tukataka kuingia kwenye ushirikiano wa uchumi na nchi nyingine zilizo nje ya EPA, mkataba hauturuhusu kwa sababu unalazimisha nchi za EAC  kupeleka kwao bidhaa zenye kuzingatia afya na usalama kwa kukidhi viwango vya nchi zao.

“Kwa mujibu wa mkataba huo, kuna uwezekano bidhaa zetu zikakosa soko kwa kutokidhi vigezo vyao pamoja na kutakiwa kuthibitisha usalama huo kisayansi ambako kwa bidhaa za nchini ni vigumu kupata uthibitisho huo kama asali inayotoka  Tabora.

“Pia, ibara ya 99 ya mkataba huo inakwenda kuua ajira kwa vijana kwa vile  inachagua ni maeneo gani ya kufanyia kazi.

“Uchumi wa nchi yetu sasa tunaelekeza kwenye mkakati wa viwanda, lakini mkataba wa EPA una mtego kwa sababu hausemi ni mazao gani ya biashara yanatakiwa kwao.

“Kwa hiyo, pamoja na Kenya na Rwanda kuusaini, bado katika jumuiya kama kuna mwenzenu mmoja hajasaini, hautasainiwa katika jumuiya husika,” alisema Profesa Kabudi.

Mmoja wa wachambuzi wa mkataba huo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. John Jingu, alisema Tanzania ikisaini mkataba huo, itapoteza mapato kwa sababu inategemea ushuru wa forodha ambao asilimia 10 ya ushuru huo, hutoka kwenye bidhaa zinazoingia kutoka Ulaya.

“EPA itaiathiri Tanzania katika biashara kwa sababu nchi inazofanya nazo biashara si za Umoja wa Ulaya kama vile Saudi Arabia, China, India, Falme za Kiarabu, Afrika Kusini, Uswisi, Marekani, Korea Kusini, Kenya na Andorra.

Awali, Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Adolf Mkenda, alisema Tanzania ikisaini mkataba huo, haitaweza kuongeza kodi na badala yake itabaki na tozo inazotoza.

Akichangia mjadala huo, Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (CCM), alisema  anaunga mkono uchambuzi wa watoa mada kwa sababu  hatua ya kukimbilia kusaini huo ni kuendelea kuumia.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msingwa (Chadema), alisema pamoja na hoja za uzalendo za wachambuzi hao, bado kuna haja ya kuelezwa pia na faida zake badala ya kutajwa hasara peke yake.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), aliitaka Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, ihakikishe inakutana na timu ya wataalamu wakiwamo wafanyabishara kujadili kwa kina mkataba huo.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger