Nov 25, 2016

Wana CCM Wazuiliwa Kumwona Magufuli


ZAIDI ya wanachama 100 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Kibaha Mjini, Mkoa wa Pwani, wamezuiwa kuingia katika viwanja vya mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OCCM), yaliyofanyika jana eneo la Bungo, wilayani Kibaha.

Tukio hilo lilitokea baada ya wana CCM hao kudaiwa kuwa hawakuwa na vitambulisho vya kuingilia katika mahafali hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa Rais Dk. John Magufuli.

Pamoja na Rais Magufuli, alikuwapo pia Mkuu wa chuo hicho, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu wa CCM, Kata ya Mailimoja, Maulid Mkwike, alisema alipata taarifa ya ujio wa Rais katika mahafali hayo juzi na kulazimika kuwajulisha wana CCM wenzake.

“Kwa hiyo, leo (jana) saa tatu asubuhi nikiwa na wana CCM wenzangu, tulikwenda katika mahafali hayo, lakini tulizuiwa kuingia getini kwa sababu hatukuwa na mwaliko.

“Wakati huo tulikuwa tumevaa sare zetu za chama, lakini tulipofika pale getini, tuliambiwa tutoe vitambulisho vya mwaliko, lakini hatukuwa navyo,” alisema Mkwike.

Akizungmzia tukio hilo, aliyekuwa mgombea udiwani Kata ya Mailimoja wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, Christopher Mjema, alisema kuwa walikwenda katika mahafali hayo kumwona Rais Magufuli kwa kuwa ni kiongozi mkuu wa chama chao.

“Magufuli ni kiongozi wetu, kwa hiyo, tulikwenda katika mahafali hayo kuonana naye. Pamoja na kwamba tulizuiwa kuingia, umefika wakati sasa uwepo utaratibu maalumu wa viongozi wa chama na hata wa Serikali, kuhudhuria katika hafla zinazofanyika katika maeneo fulani fulani,” alisema Mjema.

Naye Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kibaha Mjini, Maulid Bundala, alisema anasikitishwa na tukio la kuzuiwa kuingia katika mahafali hayo.

Wakati huo huo, Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, imeridhishwa na juhudi na mikakati inayoendelea kuelekea jumuiya hiyo kujitegemea kiuchumi kwa asilimia 100.

Kamati hiyo imefikia uamuzi huo katika kikao cha kamati hiyo kilichokaa hivi karibuni chini ya Mwenyekiti wake Sadifa Juma Khamisi katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya UVCCM, Dar es Salaam.

“Ili kuweza kujiendesha kwa ufanisi na mafanikio, kamati imeridhia uondoshwaji wa wafanyabiashara wote waliopo eneo la UVCCM  Kinondoni Mwinjuma ili kupisha uvunjaji na hatimaye kuanza kwa ujenzi wa vitega uchumi vikubwa katika eneo hilo.

“Wafanyabiashara waliopo watapewa notisi ya siku 90 ili wawe wameondoka katika eneo hilo. Uwekezaji mpya katika eneo hilo takriban kwa asilimia 99 utagharimiwa na UVCCM yenyewe,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa kufuatia tathmini iliyofanywa na UVCCM Taifa nchi nzima kwa kutathmini miradi yake kuanzia ngazi ya shina hadi taifa,  kamati imeamua na kuelekeza kuimarishwa mfumo wa ukusanyaji mapato wa jumuiya na kusimamia matumizi yake sambamba na kupitia upya mikataba yote ya uwekezaji.

Ilisema kuwa kamati ya utekelezaji imeziagiza wilaya na mikoa kutambua kuwa mali na rasilimali za jumuiya si milki ya mtu au kiongozi, kila aina ya mali au kitega Uchumi cha Jumuiya, kinahitaji kulindwa, kutunzwa na kuhifadhiwa na wanajumuiya wote hivyo imewakumbusha kuanzia sasa ni lazima kutekeleza Azimio la Siasa na Uchumi.

Source: Mtanzania


Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger