Nov 15, 2016

Wanawake Mlio Olewa na Mnaojisikia Mko Juu ya Waume Zenu Nina Kikao na Ninyi....

WANAWAKE MLIOOLEWA NINA KIKAO NA NINYI..!!
Cc: Kwa wanaume mliooa.
Mimi sio stadi wa kufundisha mambo ya ndoa kama dada yangu Rose Shaboka, lakini nikipata wasaa wa kuzungumza na wanawake walioolewa nitawaeleza neno moja kubwa ya kwamba:- wanaume tunapendezwa sana na wake walio wajasiriamali! Sio tu kwamba ninalisema mie SmartMind, hapana! Hili lina muhuri wa Mungu kama.unavyoweza kuliona pale Mithali 31.

Unajia nini? Kuna "standards" za mke mwema. Na "standards" zenyewe utabaini kwamba asilimia 98 zinahusiana na ishu za business(ama uite ujasiriamali). Huamini? Hebu angalia kidogo! Tunaambiwa mke mwema ni yule mzalishaji (anafuma, anasokota, anakusanya mazao sehemu mbalimbali n.k). Mith 31:13, 21. hii kwenye biashara tunaita, "Production". Pia mke mwema tunaelezwa anafahamu kutafuta masoko ya bidhaa zake, Mith 31:24. (yaani anaijua Marketing) na pia tunaambiwa yuko vizuri sana kwenye mahesabu Mith. 31:18 (Finance and Accounting). Yaani, huyu sio wale wanawake wanaojua kutumia zaidi ya wanachozalisha!

Ukimcheki huyu mke mwema unaona ni mwanamke mmoja mnyenyekevu sana na anaejua kufanya connections za maana, ndio maana tunaambiwa huwa anaweza kupata deals za kununua mashamba na ku-invest (Mith 31:16). Kuna ishu ya kuishi vizuri na wafanyakazi kwa ujumla wakiwemo mahausigeli. Wanawake wengi walioolewa ni watukutu sana kwa mahausigeli, lakini mke mwema tunaambiwa anafurahiwa sana na watu wa nyumbani mwake (Mith 15, 21, 27). Kwa jinsi mke mwema anavyoishi na wafanyakazi unajiridhisha kabisa ya kwamba anafahamu uongozi na utawala "Leadership and Management".

Sasa kamata pointi zifuatazo:-
1. Ukimtafiti mke mwema wa Mithali 31, unabaini kwamba ni mwanamke "milionea" mpambanaji, ambae amebaki kuwa mnyenyekevu, mwaminifu(Mith 31:11) na mtii kwa mumewe hujapata kuona!. Ndio maana tunaona mshkaji(yaani mumewe) anamumwagia masifa(mkewe) na yeye (mume) anapata masifa na promo za kumwaga town kote kwa sababu ya wife wake! (Mith 31: 23, 29). Sasa nyie wanawake mnaobahatika kupata "vielimu", tucheo ama "tuhela twa mboga", halafu mnaanza "kuzengua" kwa kuwadharau waume zetu, SmartMind nawaambia, ole wenu! By the way una uzuri gani wa maana hadi umdharau mumeo? Mke mwema wa Mithali 31 ambae ndio "Universal standard" alikuwa kawapita wote kwa uzuri (Mith 31:29) na bado alikuwa na heshima kwa mumewe, wewe umewazidi wangapi hadi unaleta ujinga huo? Mke mwema wa Mithali 31 alikuwa na contaract za biashara na wenye meli za mizigo za kimataifa (Mith 31:14), lakini wanawake wengine akibahatika kununua kagari "ka milioni nane" kama Ka-IST tu tena kwa mkopo wa ki-ajira chake, basi dharau mtindo mmoja kwa mumewe na kwa wengine! Kama wewe ni mwanamke ulieolewa na unadharau kwa mumeo, hebu nikuulize una mashamba ekari ngapi wewe hadi unaleta jeuri? Mke mwema alikuwa anapambana kuwekeza, wewe umewekeza nini na nini cha maana hadi sasa? Na upo mtindo wa wanawake walioolewa kulinganisha waume zao na wengine! Utawasikia mdomoni ama mioyoni wakisema, laiti mume wangu angekuwa kama fulani! Weee! Weee! Kuanzia leo, koma kabisa huo mtindo, ni mbaya na utakupoteza na kukusababishia uanze kumdharau mumeo. Acha kulinganisha mumeo na wengine, acha kabisa! SmartMind nikikubaini nakutandika bakora za mgongoni! Shikamana na mumeo tafuteni mali na hela, sawa enhee?

2. Hii itakushtua lakini ndio matokeo halisi ya utafiti. Huwezi kuwa na standards za mke mwema ikiwa umeng'ang'ana na kuajiriwa kwa asilimia 100 ama kuwa mama wa nyumbani tu! Kwa lugha nyepesi ni kwamba ili mke afikie standards za mke mwema ni ediha awe amejiajiri ama ikiwa kaajiriwa basi piga ua garagaza ahakikishe anajishughulisha na ujasiriamali! Kwa hiyo hapa ninatoa pole sana kwa wanawake ambao wanatamani sana kuiteka mioyo ya waume zao (kwa kiwango cha kusifiwa kama Mithali 31: 29), lakini hawana chembe ya ujasiriamali hata kidogo. Kama unabisha rudia kusoma mambo ambayo mke mwema anayafanikisha nyumbani kwake, uone kama kuna ajira yenye jeuri ya kuyatenda hayo!

Sura, shepu, rangi, make-up, mapigo ya mavazi, nywele za mitindo, hayo yenyewe huwa yapo tu:- na wala sio sehemu ya MKE MWEMA! Linapokuja suala la MKE MWEMA wanaume wote tunaburudishwa na akili za ujasiriamali alizonazo mke ama kwa lugha uliyozoea tunaita akili ya maisha. Kubweteka na sura, shepu na make-up hayo waachie michepuko huko nje, wewe ni mke, kaa mkao wa MKE MWEMA, kuwa na akili za maisha, msapoti mumeo, kuwa mnyenyekevu no matter una hela kumzidi! Kila mara lazima uwe unajiuliza, ukiacha tabia, sura, shepu, una kipi cha ziada unachofanya ambacho kinaweza kumfanya mumeo kujisifu mbele ya wenzie kwa ajili yako? Kama hujaelewa nitafute nikupatie notisi za peke yako! #SmartMind

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger