Kidunula Ameandika hivi:
Nilikuwa naangalia taarifa ya habari ITV jana sa 2 usiku, RC mkoa wa Mwanza Bw. Mongella alipokwenda kuona utendaji wa vivuko maeneo ya Ferry. Mara nikaona majibizano yafuatayo mbele ya umati wa watu.
RC MKOA WA MWANZA: Kwa hiyo wewe unavaa suti na tai unazunguka tu hapa!
BOSI WA SUMATRA MWANZA: Hapana mkuu..
RC:Nitakung"oa hapa huwezi ukawa unavaa suti tu na tai yako unazunguka zunguka tu hapa...BOSI SUMATRA: Hapana mkuu usining"oe..
RC: Nakwambia nitakung"oa hapa Ohooo.., nitakutumbua!!, huwezi ukawa unavaa suti zako na tai unazurura tu hapa halafu watu wanakuona we wa maana kuliko mimi..!
BOSI SUMATRA: Hapana usining"oe mkuu..
RC: Huwezi ukawa unapokea mshahara unakula wewe na mkeo halafu mimu nije nifanye kazi zako hapa, mimi siyo mtaalamu wa haya mambo..!
Bosi wa SUMATRA akaishia kujitabasamlisha huku mikono ikiwa haitulii,na macho yake yakiwa ni yenye fedheha fulani.
Kiukweli nilimuonea huruma sana manake naamini ndugu zake,rafiki, na familia yake walikuwa wanaangalia hyo taarifa ya habari.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment