Akaja mliyekuwa mnampinga kwa nguvu zenu zote kwa miaka minne, akawapima akajua mna njaa, akawapa kauli mbiu ya safari ya matumaini, akajua elimu hamna, akawapa matumaini ya ELIMU, ELIMU, ELIMU kwa kuiweka elimu ya mtoto wa miaka mitatu hadi wa miaka hamsini, yaani chekechea hadi chuo kikuu kwenye chungu kimoja japo elimu hiyo imegawanyika katika elimu ya awali, hadi elimu ya juu ila yeye kachanganya sehemu moja yote! Yaani ni sawa na uwaweke wanafunzi wote kuanzia chekechea hadi chuo kikuu darasa moja halafu uwafundishe wimbo: ELIMU, ELIMU, ELIMU na wote wanaitikia!
Maji ukiyapiga kwa fimbo au kitu chochote, hayatawanyiki kuelekea upande mmoja, bali pande zote. Hivyo ujio wa Lowasa Chadema uliwatawanya wanachama wake, wapenzi na mashabiki. Katika mtawanyo huo, wapo waliorudi na kuenda naye kwenye kuzungusha mikono a.k.a safari ya mabadiliko, pia wapo ambao baada ya kutawanywa hawakurudi hadi wa leo.
Mtawanyo huo ndiyo mwanzo wa kushindwa kwa upinzani na CCM kuendelea kubaki madarakani. Ndiyo maana Simba katika mawindo yake, kama anakimbiza swala, halafu akakutana na nguruwe, ataendelea kumkimbiza swala hatahangaika na nguruwe. Hii ina maana mahali Bavicha walipotea ni hapa kuacha kukimbiza swala waliyekwishaanza kumkimbiza na kukimbiza nguruwe na mwishowe wakakosa wote na hii inadhihirisha wanyama kama simba wana akili kuliko Bavicha huku Mwenyezi Mungu ametupa utashi wa kutawala wanyama hao.
Bavicha kama hamuamini lengo la Lowasa ni kuendelea kuibakiza CCM madarakani miaka 50 ijayo kama alivyowatamkia, basi endeleeni na safari ya kuelekea 2020 na Lowasa muone tena kichapo toka CCM. Kwa leo ni hayo tu, nawatakia tafakari njema
Maoni Huru Kutoka Kwa Sirluta/JF
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment