Waandishi wetu waliokuwa katika vituo mbalimbali kushuhudia majaribio hayo walishuhudia abiria wengi wakishindwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na wahusika ikiwamo wasio na matatizo kuketi kwenye viti vya wenye ulemavu.
Pia, wapo walioonekana wakizunguka na mabasi hayo kutoka kituo kimoja hadi kingine bila kushuka hadi walipoteremshwa kwa nguvu.
Juzi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Udart, Ronald Lwakatare alisema mabasi 140 yangeanza kubeba abiria bure jana na leo katika majaribio.
Baadhi ya maofisa waliokuwa wakitoa elimu juu ya matumizi ya mabasi hayo, walisema kuna changamoto ya wakazi hao kuelewa haraka mfumo wa malipo.
Kwa mujibu wa maelekezo ya maofisa hao, kila abiria atatakiwa kufuata hatua mbalimbali kabla ya kupanda usafiri huo na kushuka.
Hatua hizo ni kulipa na kupewa kadi ambayo ndiyo itakayotumika kuingia na kutoka katika kituo. Abiria wote wanapaswa kutumia mlango wa mbele au nyuma wakati wa kuingia kwa kugusisha kadi hiyo ambayo ndiyo inayofungua mlango.
Baada ya kuingia, basi linapofika kituoni, mlango yake hufunguka sambamba na ilipo ile ya kituoni hivyo kutokuwa rahisi kwa mtu yeyote kupenya. Katika utaratibu huo, ni vigumu kwa abiria kuingia na kutoka bila kulipa kutokana na mfumo huo.
Wakazi wanena
Wakazi wa maeneo ya Ubungo, Kinondoni, Kivukoni, Kimara na Kariakoo waliozungumzia usafiri huo walieleza kuridhishwa kwao na mfumo huo wa malipo licha ya baadhi yao kusema una mzunguko.
Mkazi wa Kigamboni, Mashaka Seif alilalamikia usafiri huo kuchelewa kuanza alfajiri kama ilivyotangazwa, hatua iliyoathiri wengi kufika kwenye maeneo yao ya kazi.
Imeandikwa na Colnely Joseph, Suzan Shayo na Kelvin Matandiko
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment