Akizungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi amesema watafuata taratibu zote za kisheria ikiwamo kutoa taarifa na kuomba ulinzi wa polisi.
Katambi amesema ajenda za mikutano hiyo zitakuwa ni kupinga ukandamizaji wa demokrasia nchini, pamoja na kupinga hatua ya viongozi wa vyama vya siasa kukamatwa na polisi mara kwa mara bila sababu za msingi.
"Wote tunaona jinsi Serikali inavyoingilia mihimili mingine. Mahakama ndiyo chombo pekee ambacho kinatoa haki, kama mhimili huu unaingiliwa basi hata hukumu zinazofanyika zitakuwa za mashaka," amesema Katambi.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment