siku mbili zilizopita nilisafiri kwa shughuli za kiofisi. Kama mjuavyo mambo ya serikali yetu hii, unajaza imprest, hela ya safari inachelewa kutoka, au unaweza kulipwa hata baada ya wiki au mwezi tangu urudi toka safari. Sasa mimi ndo yakanikuta. Ikabidi nijiongeze tu ili kuokoa ratiba zangu. Na kumbuka ni tarehe za karibia na mishahara. Nikaacha hela ya mahitaji, nikasisitiza kuwa tusifanye manunuzi yasiyo ya lazima kwa sababu tuko kwenye ujenzi na mafundi hivi wanatudai, hivyo mshahara ukitoka tu tuwalipe. Leo ndo nimerudi kutoka safarini na leo ndo mshahara umetoka. Nilikuwa nimechoka sana leo. Asubuhi nilikunywa kikombe cha maziwa na maandazi mawili, nikashinda nayo njia nzima mpaka nimefika home mida ya saa kumi na nusu. Tangu asubuhi nilijihisi siko vizuri kichwa kinaniuma, najisikia kuchoka. Nikiwa nimekaribia home nikampigia wife kuwa nakaribia kufika. Nashukuru nilifika salama. Njiani nikanunua vitu mbalimbali kama matunda na mboga.
Sasa kilichonifanya niwaze sana kuhusu hawa viumbe wanawake, nilipofika nilisalimia walio nje, then nikaingia ndani. Nikamkuta yuko chumbani amelala. Baada ya salamu, nikarudi nje binti wa kazi alikuwa anaosha vyombo. Nikakaa sebuleni kama dakika 10 nikaona hakuna anayekuja siyo yeye wala msichana. Nikachukua glasi nikanywa maji, nikarudi kukaa kwenye sofa. Nikaona watu wako bize na ratiba zao, Nikatoka nje binti bado anaosha vyombo. Nikarudi ndani chumbani. Nilipoingia nilikutana na swali, "mshahara wako umetoka?"Nikajibu ndiyo. Akasema "hata mimi wa kwangu umetoka, sasa naomba niongezee laki mbili niende mjini sasa hivi kuna nguo nataka nikanunue".
Niliwaza tuu haraka hata sijapewa maji ya kunywa, wala sijaoga niko na jasho la safari, hata sijapumzika, kichwa kinaniuma, njaa inaniuma (maana huwa sipendi sana kula hovyo hovyo njiani), hata hajaniuliza safari ilikuwaje; Nilijisikia kizunguzungu flani cha ghafla, nikatoka nikafunga mlango, nikaondoka zangu nikawasha gari kwenda mjini kutafuta sehemu ya kupumzika walau nipate hata uji au supu nipashe tumbo.
Mpaka sasa sijarudi nyumbani, nasubiria muda uende nikifika naoga nalala tuu. Inaniuma sana, hivi vitendo siyo mara ya kwanza. Mpaka sasa ana masanduku matatu makubwa yote yamejaa nguo zake bado anaona hana nguo, eee Mungu uwarehemu hawa viumbe. Mimi nawaza tumalizie ujenzi tuachane na nyumba ya kupanga, yeye wala haoni kama kuna shida. Alafu sisi wanaume tukichepuka tunalaumiwa sana na hawa wanawake kuwa tunatelekeza familia. Anyway, nafikiria kitakachotokea nikirudi nyumbani
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment