Tukio hilo lilitokea mwezi ulioisha wa Julai, ambapo Imamu huyo alijikuta akitamka maneno 'YESU NISAIDIE' pale alipokuwa akiongoza swala ya alfajiri katika siku ya kwanza ya Jumatatu, ambapo waumini aliowaongoza walimuonya kwa kitendo hicho. Hali hiyo ilimrudia siku hiyo hiyo ya Jumatatu, safari hii alipokuwa akiongoza swala ya alasiri. Waumini walimpa onyo, lakini yeye alijitetea kwamba alikuwa haelewi kama ameyatamka maneno hayo.
Kama vile haitoshi, siku ya pili yake (Jumanne) Imamu huyo alijikuta akirudia kwa mara ya tatu kutamka maneno 'YESU NISAIDIE', jambo ambalo halikuvumiliwa tena na waumini wa msikiti huo ambapo walichukua uamuzi wa kumtimua katika msikiti huo na kumtaka kukabidhi mali alizokuwa amepewa, ikiwemo simu
Baada ya hapo baadhi ya marafiki na ndugu zake walimtenga na kumuona sio mwenzao tena, ambapo alijihifadhi kwa nduguye mmoja huku akiwa na kanzu tu. Ndipo usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, hamu kubwa ya kumpokea Yesu kwa kwenda kanisani ilimjaa, na alitimiza adhma yake kwa kuhudhuria misa akiwa amevaa kanzu yake katika kanisa hilo la TAG Magomeni, na kupokelewa vizuri na waumini wa Kikristu wa kanisa hilo
Imamu huyo amedai kwamba kuna waumini kadhaa huwa wanapata maono juu ya Yesu Kristu kwa namna tofauti, lakini wamekuwa ni waoga kumpokea Kristu kwa hofu ya kutengwa na jamaa zao
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment