TCRA wanasema Clouds Media imepigwa faini hiyo kutokana na kosa la kushabikia mapenzi ya mbuzi na binadamu kwenye chombo chao cha habari na kupiga wimbo wa mwanamuziki Mwana FA ambao unapaswa kupigwa muda maalumu ambao wameagizwa.
ITV wamepigwa faini hiyo kutokana na kipindi kutoka bungeni kilichokuwa kinaoongozwa moja kwa moja,ambapo Mbunge wa Iringa Mjini alisikika akisema “Naibu Spika amekuwa kama anavaa pampas,hataki kubanduka kwenye kiti kuongoza bunge”.
TCRA imewakumbusha wadau wote kufuata sheria na maadili ya utangazaji ili kuepuka adhabu na ukiukwaji wa maadili.
Source: Mwananchi/Jamii Forum
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment