Tundu Lissu |
Licha ya Tundu Lissu kumtukana Rais hadharani, hakuna aliyemtoa hata ngeu. Alikamatwa kistaarabu. Akasafirishwa kistaarabu toka Singida hadi Dar es Salaam na akafunguliwa mashtaka kistaarabu. Kubwa zaidi ni pale mkondo wa sheria ulipopewa nafasi kwa Tundu Lissu kupewa muda wa kutosha kujitetea hadi kesi yake kuvunja rekodi ya kusikilizwa kwa zaidi ya dakika 500. Haya yote hayajapatapo kutokea kwenye utawala wa kidikteta.
Kikubwa zaidi ni pale Tundu Lissu alipopata dhamana na sasa yupo uraiani. Sidhani kama kwa nchi za kidikteta leo hii angeliona jua.
Niwakumbushe ndugu zangu wa upinzani kwamba siasa si ugomvi na wala si uadui. Lowasa amewafundisha muwe na siasa za kistaarabu na kimikakati kama kweli mna dhamira ya kwenda Ikulu. Kinyume chake mtaendelea kuwa wasindikizaji kwani sisi wananchi wa kawaida tunaendelea kuwadharau. Na ndio maana kila awamu kunakuwa na mabadiliko ya chama kikuu cha upinzani lakini CCM inaendelea kujinafasi kileleni. 1995 hadi 2000 tulikuwa na NCCR Mageuzi. 2000 hadi 2010 tulikuwa na CUF. 2010 hadi sasa tuna CHADEMA. Sitashangaa kuona mwaka 2020 tukiwa na chama kingine kikuu cha upinzani.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment