Kamanda Sirro |
Ilitegemewa kuwa, Jeshi la Polisi lingetoa taarifa rasmi juu ya mapambano ya kurushiana risasi baina ya polisi na wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, hata hivyo jeshi hilo limesema, “operesheni inaendelea. Hatuwezi kutoa taarifa juu ya kilichotokea jana.”
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Siro, amewaambia wanahabari leo kuwa, askari zaidi ya 80 wamepelekwa katika operesheni maalum ya kuwasaka majambazi katika misitu inayounganisha mikoa ya Pwani na Dar.
“Wakati oparesheni inaendelea mimi siwezi kutaja nani kapata nini na kwa wakati gani. Kufanya hivyo ni kinyume na taratibu zetu za kazi, kuwa kwenye oparesheni huku unatoa taarifa muhimu,” amesema.
Kwa mujibu wa Sirro, oparesheni hiyo ni mwendelezo wa mapambano kati ya askari wa jeshi hilo na wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliofanya mauaji ya askari wanne katika tawi la benki ya CRDB lililopo Mbande jijini Dar es Salaam.
“Tumeanza Oparesheni juzi, jana na leo tunaendelea naamini ikifikia Jumanne tutawapa majibu sahihi. Niwahakikishie kwamba silaha zitarudi,” amesema Kamanda Sirro.
Hapo awali, taarifa zizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari hususani asubuhi ya leo ambazo bado hazijathibitishwa na jeshi hilo zimesema, Kamishna wa Kitengo cha Kuzuia Ujambazi, ASP Thomas Njuki aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani wakati wa mapambano hayo lakini pia jambazi mmoja akiuawa katika mapambano hayo.
Mwanahalisi
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment