Wazee wa CUF |
Waheshimiwa Waandishi wa habari, Wananchi na Wanacuf.
Sisi Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam tunapenda kuwajulisha kwamba, tulichukua hatua kadhaa za kushauri juu ya kadhia hii iliopo ndani ya Chama chetu kwa sasa bila Mafanikio.
Ukosefu wa Mashirikiano mema, Kibri, Jeuri na ubinafsi ndani ya Viongozi wa Chama Chetu ndio uliozaa kilichotokea pale Ubungo Plaza Tarehe 21/08/2016.
Kutengwa kwa baadhi ya viongozi na kuporwa kwa Majukumu yao ya Kiutendaji ndani ya Chama, kutokubali ushauri wa Wazee Kuhusu kumaliza kile kinachoitwa Mgogoro wa Kujiuzulu Prof Ibrahim Haruna Lipumba ndio chanzo kikubwa cha Mpasuko ndani ya Chama chetu.
Sisi Kama Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam tutaona Kuna Mkakati wa Makusudi unaofanywa na Katibu Mkuu wetu Maalim Seif Shariff Hamad wa kukiua Chama cha Cuf kwa upande wa Tanganyika. Hakuna Tatizo la Kikatiba katika kumaliza Mgogoro huo. Ibara ya 117 kifungu cha 1 na 2 kinaeleza vyema utaratibu wa Kujiuzulu, na kwa kweli Wajumbe wa Mkutano Mkuu walitekeleza Wajibu wao.
Sisi Wazee tunapenda kuwajulisha Watanzania kwamba, tulikutana na Katibu Mkuu, na tumemnasihi sana amalize tatizo la Prof, lakini kama tulivyosema hapo awali kwamba Kibri, dharau na Jeuri ndio vimetufikisha hapa.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wapatao 324 wamewasilisha Madai yao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kupinga Ubeberu huu unaofanywa na Katibu Mkuu, sisi Kama Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam tunaunga Mkono maamuzi hayo.
Na tunatoa wito kwa Msajili kushughulikia tatizo hili kwa Mujibu wa Katiba yetu. Ni fedheha kubwa kwa sisi tunao hubiri Demokrasia kuiminya Demokrasia ndani ya Vyama vyetu.
Kuhusu Vikao vilivyoitishwa leo na Katibu Mkuu kwa kushirikiana na Viongozi wa Zanzibar tu, bila kushirikiana na Viongozi wa Bara, sisi Kama Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na uzoefu wa kilichotokea kwenye Mkutano Mkuu uliofanyika pale Ubungo Plaza Tarehe 21/08/2016 tumeamua kuwakataza Wajumbe wetu wa Baraza Kuu toka upande wa Bara, ambao wamejitoa Muhanga kupinga Ubeberu huu, kuto hudhuria Vikao hivyo kwakua Hatuna uhakika wa Usalama wa Vijana wetu.
Mwisho tunatoa wito kwa Katibu Mkuu wetu, kama ambavyo tulimueleza kwenye Kikao chetu, na leo tunarudia tena, ni vyema akamaliza tatizo hili kwa busara ili kuondosha Mpasuko uliojionyesha wazi wazi wa Ubara na Uzanzibar.
Hatutakubali kufukuzwa kwa Mwanachama yoyote yule eti kwakua tu Wanapingana na Maalim Seif Shariff Hamad na Genge Lake.
Abdul Rajabu Magomba.
Katibu wa Wazee mkoa wa Dar es salaam
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment