Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema kitendo cha Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kuendelea na mikutano ya kisiasa mikoani na kuwazuia viongozi wa vyama vingine vya siasa ni kutaka kukwamisha demokrasia nchini.
Akizungumza jana katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na Televisheni ya Azam, Mbatia alisema Rais Magufuli akiwa Singida, aliviponda vyama vya upinzani kuwa vimekufa.
“Akiwa Singida Magufuli alisema vyama vya siasa vya upinzani vimekufa na kuvilinganisha na nyoka aliyekanyagwa kichwa na kubakiwa na mkia tu unaocheza cheza,” alisema.
Alisema Agosti 12, mwaka huu Magufuli alikuwa mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam akizungumza na wanachama wake na kuonyeshwa na televisheni mbalimbali akikijenga chama chake.
“Nani anakwenda kuweka rekodi vizuri huko mikoani kwa anayoyasema Magufuli kama anazuia wapinzani wasifanye siasa? Kwa hiyo yeye anajenga chama chake lakini anazuia wapinzani wasifanye hivyo,” alisema.
Alisema ikumbukwe kuwa Tanzania ni ya watu wote na wanatakiwa kufuata sheria na utaratibu uliowekwa na si vinginevyo.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment