Aug 22, 2016

Wassira Aiomba Serikali Izungumze na Chadema ili Kumaliza Malumbano


Aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Chakula na Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wassira ameomba wasaidizi wa Rais John Magufuli kumshauri kufanya mazungumzo na viongozi wa upinzani ili kuepusha madhara yanayoweza  kutokea kutokana na maandamano yanayopangwa kufanyika Septemba 1.


Wassira ameeleza kuwa washauri hao wanapaswa kufanya hivyo kwani bado nafasi hiyo ipo kuliko kuacha Rais aingie vitani na wananchi wake kwani madhara yatawapata Watanzania wote.


“Wazungumze ili wasimuingize Rais kupigana na watu wake kwa maana wote tutapoteza. Kwa nini uweke askari polisi wote hao, msimweke Rais kwenye vita na watu wake,” Wassira anakaririwa na Jambo Leo.


“Kinachohitajika ni wasaidizi wa Rais kumshauri ili kuhakikisha kuwa tofuati zilizopo baina yake na vyama vya upinzani haziendelei ili kuepusha madhara yanayoweza kuzuilika, itafutwe suluhu,”aliongeza.


Akizungumzia uamuzi wa Serikali kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano na maandamano, alisema kuwa tatizo linaweza kuwa ni aliyekuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.


Alisema kuwa hii inatokana na joto la uchaguzi lililokuwepo pamoja na nia ya Lowassa kuzunguka nchi nzima kuwashukuru wapiga kura, kungeweza kuzua tafrani kubwa kwani alipata kura nyingi na alikuwa akidai ameshinda kwa asilimia 62.


“Ukiwaruhusu kufanya mikutano na ukwaambia kuwa atakayekuja kutoa shukurani ni Lowassa, ambaye amekuwa akipinga kushindwa ni sawa na kurejesha hali ya uchaguzi kipindi hiki,” alisema.


Alitaka Serikali kutoa elimu ya wazi kwa umma kuhusu sababu zinazopelekea kukataza kufanyika kwa mikutano ili kuweka mambo sawa.


“Kama mimi hapa nimetaja sababu kwamba inawezakana kuwa ni Lowassa. Sasa na wao Serikali waseme tu tunapiga marufuku mikutano na maandamano… wataje [sababu]na kuzifafanua,” alieleza.


Hata hivyo, Wassira aliwataka Chadema kusitisha adhma yao na kuhakikisha wanafuata utaratibu ili kupata haki ya kufanya maandamano na mikutano ambayo alieleza kuwa kila Katiba ya nchi duniani imeiweka, lakini bila kufuata utaratibu haiwezi kuruhusiwa.


Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger