Moja kati ya swali ambalo aliulizwa muimbaji huyo na mmoja kati ya wanafunzi wao, kwanini anavaa nguo zisizo na maadili kwenye video zake wakati wanaweza kuvaa nguo za madela ambazo amedai ni za heshima.
Katika kujibu swali hiyo, Lady Jay Dee alisema binafsi yeye hawezi kuvaa madela na ni nguo ambayo haipendi kuvaa.
“Mimi sipendi kuvaa madela kwa hiyo siwezi kuvaa dela kwenye wimbo wangu,” alisema Lady Jay Dee “Na mimi naamini sanaa unafanya kile kitu ambacho uko huru nacho na unakifanya kutoka moyoni,”
Pia muimbaji huyo amesema yeye anaamini mashabiki wake wanampenda vile anavyofanya ndio maana mpaka sasa anaendelea kufanya vizuri kwenye muziki wake.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment