Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa CCM katika Kata ya Sambasha wilayani Arumeru mkoani Arusha alikamatwa na polisi Septemba 16 na alikaa rumande kwa mahojiano hadi leo alipofikishwa mahakamani.
Mwendesha mashitaka wa serikali, Lilian Mmasi alieleza mahakama kuwa, Sabaya alitenda kosa la kwanza Agosti 13 mwaka huu, katika nyumba ya kulala wageni ya Skyway jijini hapa.
Alisema alijifanya ni mtumishi wa Usalama wa Taifa wa kujipatia huduma mbalimbali kwa njia ya udanganyifu.
Alisema katika kosa la pili, katika muda usiojulikana, Sabaya anatuhumiwa kugushi kitambulisho cha Usalama wa Taifa namba MT.86117 wakati akijua ni kosa la jinai kufanya hivyo.
Baada ya maelezo hayo, Sabaya alikana makosa hayo na wakili wake, Yoyo Asubuhi alimuomba hakimu mkazi Gwantwa Mwankuga ampatie dhamana mteja wake.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment