NIKKI MBISHI - KAMA BABU TALE NDIO MWENYE
MUZIKI BASI #BABU_TALENT INAMUHUSU
Rapper Nikki Mbishi amefunguka kuhusu wimbo wake ujao,
‘Babu Talent’ ambao anadaiwa kumuimba @Babutale kwa
asilimia 100.
Akiongea kwenye kipindi cha E News cha EATV, rapper huyo
amedai kuwa wimbo huo unaweza ukamgusa meneja huyo
wa #Diamond kwa asilimia ambazo yeye mwenyewe
anazoweza kuzihisi.
.
“Yeye ni mwenye muziki kwahiyo?,” aliuliza @Nikkimbishi.
.
“Wamejiongeza wao, ni sawa sawa na kumuimba Nay Wa
Mitego, mimi nilimuimbia mwanamke sasa nyinyi mnamjua
#NayWaMitego huyo ni wa kwenu nyie.”
.
“Ngoma very soon inakuja watu wakae tayari sasa hivi kwa
maandalizi kwa sababu nafanya version za Babu Talent
tofauti tofauti. Kuna moja imeshafanyika kuna nyingine bado
session zipo kwa sababu watu wengi wameniomba kuniofa
mdundo wa kufanya hiyo kitu,” aliongeza.
#letitshine
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment