Mbali na Muganyizi washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Maseke Zenge (50), Mhasibu Augustine Mrema (55) na Ofisa wa Kampuni ya udalali ya Unyangala Auction Mart, Ahadik Kambona.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai mbele ya Hakimu Mkazi Emmillius Mchauru kuwa katika tarehe isiyofahamika washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa.
Aliendelea kudai kuwa, Juni 19, 2014, wakiwa Dar es Salaam kwa nia ya udanganyifu, washtakiwa walighushi mhuri wa benki hiyo kuonesha amri ya kukazia hukumu imepokelewa na benki hiyo huku wakijua si kweli.
Katika shitaka la tatu inadaiwa, siku hiyo, washtakiwa walighushi saini ya Ofisa wa benki hiyo kuonesha ametia saini kupokea kikazia hukumu jambo ambalo si kweli.
Aidha, inadaiwa Agosti 22, 2014 wakiwa kwenye jengo la NMB katika mitaa ya Azikiwe na Jamhuri waliwasilisha kwa Ofisa wa Sheria NMB nyaraka hiyo kuonesha imetolewa na Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Kisutu huku wakijua si kweli.
Katika mashitaka mengine inadaiwa, washtakiwa wakiwa katika jengo hilo kwa njia ya udanganyifu walijaribu kujipatia Sh milioni 51,640,000 kutoka kwenye benki hiyo, baada ya kudanganya kuwa hukumu ya benki hiyo inapaswa kulipa fedha hizo zilizoandikwa kwenye kikazia hukumu.
Washtakiwa walikana kuhusika na makosa hayo na Wakili Katuga alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Washtakiwa waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili waliosaini hati ya Sh milioni 10. Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 5, mwaka huu.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment