Samatta ambaye alianzia benchi na kuingia kipindi cha pili dakika ya 67 kuchukua nafasi ya mjamaica Leon Bailey, alishuhudia timu yake ya KRC Genk ikiwa nyuma kwa goli 2-1 hadi alipoingia kwenda kuongeza nguvu dakika ya 78 akafanikiwa kutoa assist na kuinusuru KRC Genk isipoteze mchezo wa tano wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu huu.
Kufuatia matokeo hayo KRC Genk inakuwa nafasi ya 9 katika msimamo wa Ligi Kuu Ubelgiji, magoli ya KRC Genk yote yalifingwa na mgiriki Nikolaos Karelis dakika ya 33 baada ya kutumia vyema pasi ya Pozuelo na 78, wakati magoli ya Mouscron yalifungwa Hassan Mahmoud dakika ya 3 na Valentin Viola dakika ya 42.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment