Oct 31, 2016

Nyuma ya Pazia Diamond Kumfunika Kiba kwa ‘Yai’


MWISHONI mwa wiki iliyopita, gumzo kubwa kunako tasnia ya burudani Bongo ilikuwa juu ya hafla ya utoaji Tuzo za MTV Afrika (MAMA) ambapo wawakilishi kutoka Bongo, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, Navy Kenzo, Yamoto Band, Diamond, Raymond na Ali Kiba ‘King Kiba’ walitoka kapa.

Mengi yameongelewa kuhusiana na tuzo hizo kuonekana kama zilitolewa kwa upendeleo (Sauz na Nigeria) huku chache zikitolewa kwa nchi tofauti za Afrika.

Ukiachilia mbali wawakilishi wetu kuambulia patupu, mapema kabla ya kuanza kwa hafla hiyo, King Kiba pamoja na Sauti Sol kutoka Kenya walialikwa kwenye mahojiano juu ya muziki wao. Kiba alionekana mtu wa kutojiamini ambapo alikuwa akirudia neno ‘you know’ mara kwa mara.

Mbali na hiyo yakaja mahojiano ‘red carpet’ dakika chache kabla hafla hiyo haijaanza, napo Kiba alionekana kujiumauma huku msanii mwenzake Diamond akionekana kumfunika kwa kutema ‘yai’ (Kiingereza) lililokomaa.

Japokuwa yai bovu la Kiba liligeuka gumzo kubwa mitandaoni ni ukweli ulio wazi kuwa Diamond wa zama zile si Diamond huyu, Kiba wa kipindi kile anaweza kuwa Kiba huyuhuyu. Namaanisha kwamba, Diamond alijipanga kuwa wa kimataifa lakini Kiba hakujipanga zaidi ya kuonekana kama mtu aliyelala na kuamshwa ghafla na nguvu za mashabiki.

Katika makala haya, yapo mambo yanayoonesha wazi vitu vilivyochangia Diamond kumfunika Kiba katika kutema yai.

Kujichanganya

Tangu Diamond ameanza muziki, amekuwa ni mtu wa kuangalia mbele. Kujitoa ufahamu na kujichanganya mbele za watu wenye mafanikio kumemfanya kufikia hapa alipo.

Ikumbukwe kuwa Kiba ndiye aliyeanza kujulikana kimuziki kisha Diamond akafuata lakini alivyofuata hakusimama, alipiga hatua kuanzia alipopata shavu la kuwa karibu na Bob Junior (Sharobaro Records), Prof. Jay, AY, Davido (Nigeria) na sasa Ne-Yo (Marekani).

Kila ngazi aliyokuwa akipitia alihakikisha anajiamini kwanza pasipo kuogopa, kitendo cha kukutana na Davido katika Tamasha la Fiesta, 2013 kilimuonesha ukomavu wa kujua kutema yai ambapo alitimba Nigeria na kutema yai na wengi wakiwemo Iyanya, KCEE, Bracket, Tiwa Savage, Korede Bello, P-Square na sasa anatema na Ne-Yo bila kujiumauma.

Upande wa Kiba, kwa muda mrefu amekuwa si mtu wa kujichanganya na wenzake wa kimataifa, ukiangalia katika kazi za nje ya nchi alizofanya ni wazi utazungumzia ya zamani (One8) aliyofanya na R. Kelly na baadhi ya wasanii wa Afrika mwaka 2010 na hadi leo hakuna chochote.

Mastaa aliotoka nao kimapenzi

Siri nyingine ya Diamond kumfunika Kiba kwa yai inatokana na mastaa aliotoka nao kimapenzi ambao ni Wema, Penny, Jokate na sasa Zari.

Diamond alipoanzisha uhusiano na Wema hakuwa akijua kutema yai kiufasaha na alishawahi kukiri kufundishwa na Wema. Alipomwagana na Wema, alimpata Mtangazaji Penny ambaye naye kwenye yai yupo fiti jambo lililomfanya kukuza yai lake.

Baada ya kutemana na Penny, akaangukia kwenye penzi la Jokate ambaye naye kwenye yai yupo fiti, akaendelea kujipiga msasa japo kwa kujiumauma. Hakudumu sana na Jokate akarudi kwa Wema kisha akaangukia kwa mrembo kutoka Uganda, Zari ambaye amezaa naye mtoto mmoja hadi sasa.

Lugha kuu ya Zari ni kutema yai kuliko kuzungumza Kiswahili na hili limemfanya Diamond kukomaa zaidi na kujiamini pale anapoulizwa kitu na mtu anayejua yai.

Ukija kwa Kiba napo ukiondoa uhusiano wake na Jokate ambao si wa uhakika kivile, anadaiwa kuzaa na wanawake tofauti ambao kwao yai limepita kushoto hivyo kumfanya asiwe mkali katika kulitema.

Malengo

Diamond tangu aanze kutoka kimuziki alijua siku moja atakuja kuwa wa kimataifa, akaanza kujiandaa mapema kwa maana ya kujiweka kistaa kuanzia muonekano hadi kwenye kutema yai.

Licha ya kupata shavu la kufundishwa na watu aliokuwa nao katika uhusiano, Diamond pia ametumia fedha kutafuta walimu wa kumnoa ambapo hadi sasa katika lebo yake ya WCB wasanii wake wengi wamenolewa.

Ukija kwa Kiba japo ni msanii mkongwe, inaonekana hakuwa na malengo ya kufika mbali zaidi. Alitamba miaka ya mwanzoni mwa 2000 lakini akapotea, nguvu za mashabiki zikamrudisha tena baada ya kuanzisha Kampeni ya ‘Bring Back Our Mc’. Alivyorudi hakuwa amejiandaa kimataifa bali kuonesha uwepo wake na kipaji chake.

Ushauri

Kiba ni miongoni mwa mastaa wakubwa nchini, ana kipaji cha hali ya juu na ndiyo maana lebo kubwa duniani (Sony) imemuona na kumsainisha. Kinacho-muangusha ni kutoji-amini nafasi aliyonayo (ustaa) kama anaweza pamoja na kukubali kujifunza kila siku, kama yai linaonekana kuwa gumu kidogo kwake zipo njia za ‘kusolve’ na akapigwa msasa akawa sawa.



Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger