Ghalama ya kila kiti ni shilingi laki mbili,hivyo kwa jumla ya ghalama ya viti tu bila mageti ni karibu milioni 300.Mh.Nape Nnauye anasema Rais amekasirika sana kwa kitendo hicho na alitaka adhabu iwe kali zaidi lkn wakaamua kama serikali ni kufungia Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka hapo serikali itakaposema vinginevyo.Pia serikali imeamua kuzuia mapato yote ya Simba na Yanga mpaka hapo watakapothibitisha kulipa uharibifu wote uliofanywa na mashabiki wao.
Mh.Nnauye anasema wataenda mbele zaidi kwa kuweka kamera uwanjani ili waweze kunasa sura za mashabiki watakaokuwa wanafanya vitendo vya uharibifu.
Chanzo kikubwa cha vurugu katika mechi ya jana ilikuwa ni mambo mawili;kwanza ni mfumo wa kadi kufeli,kadi nyingi "ukichambisha" zilikuwa zinasema kadi fake na hapo mtu katoka kununua kwenye kituo halali na kwa watu halali,na kadi nyingine zinasema huna salio la kutosha.Na hata ukienda kwa polisi basi unaambulia kirungu au kofi kwa kudhaniwa ni "usanii"
.Hali hii ndio ilisababisha watu waanze kuvamia mageti kwa kuona hakuna namna.Kadi umekata na uwanjani usiingie.Serikali imtazame upya mzabuni aliyepewa kazi ya kuuweka mfumo wa kielectroniki ambaye majaribio yake ilikuwa ni mechi kubwa ya Simba na Yanga.Mfumo ulionyesha kushindwa kabusa kabisa.Mpaka saa kumi jioni,upande niliokuwepo watu karibu 500 kadi zao zilikuwa zinagoma.
Sababu ya pili ni Refa Saanya.Huyu maamuzi aliyoyafanya anastahili adhabu.Hili si la kuongelea sana maana lipo mikononi mwa bodi ya ligi,TFF na Chama cha Waamuzi.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment