Kimsingi TFF haipingi mabadiliko ya aina yoyote, badala yake inataka kujua kama taratibu hasa zinazohusiana kisheria kama zimefuatwa hivyo sasa imeitisha mkataba huo kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans, Bakara Deusdedit ili kuona kile kinachoelezwa kuhusu mfumo wa uendeshwaji na umiliki wa klabu hiyo yenye zaidi ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.
“Msimamo wa TFF ni kwamba klabu ya Yanga ipo kama ilivyokuwa kwa mujibu wa taratibu za TFF, CAF na FIFA hadi hapo tutakapopopata barua kutoka Young Africans na wanatambua uongozi wa Mwenyekiti Yussuf Manji na Kaimu Katibu Mkuu Deusdedit Baraka,” amesema Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine.
TFF imekuwa ikipokea barua kutoka kwa wadau mbalimbali wa Yanga wakihoji taratibu au hatua zinazoendelea katika mfumo wa umiliki na uendeshwaji wa timu hiyo. Mbali ya hatua hiyo, Alhamisi iliyopita ya Oktoba 6, 2016 vyombo mbalimbali vya habari vilikuwa na taarifa kuhusu muhtasari wa mkataba wa Yanga wa kukodishwa na kampuni ijulikanayo kama Yanga Yetu Limited.
Mbali ya misukumo hiyo, pia TFF haikuridhika na majibu ya Kaimu Katibu Mkuu wa Young Africans, Bakara Deusdedit ambaye alipoandikiwa barua kwa mara ya kwanza Agosti 30, 2016 alitoa majibu kwamba awasiliane na wajumbe wa Bodi ya Udhamini.
Mwesigwa amesema wanataka kuona kilichopo kwenye mkataba kabla ya kushauri uongozi ili kuangalia kama vinakwenda sambamba na matakwa ya TFF, CAF na FIFA ili kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakiendelea kwani wengine wamefika hatua ya kuomba idhini ya TFF hata kwenda kuwaona viongozi wa serikali.
Mwesigwa alisema wanataka kujua pia nani anamiliki na nani anaendesha timu na umiliki wake ukoje kwa maana hizi timu za Simba na Yanga zinagusa nyoyo za watu wengi na taratubu za uhamishaji umiliki wake ukawa wa wazi-hadharani.#
“Mambo ya kubadilisha uendeshwaji unatakiwa kufuata taratibu ikiwa ni pamoja kuenenda sawa na katiba ya klabu, kamati ya utendaji ifahamu, mkutano mkuu uridhie ili kujua nini kinauzwa na nini kinakodishwa ikiwa ni kwenye level (hatua) ya klabu.
“Kama itakuwa nje ya utaratibu wetu wa uendeshaji wa klabu kamati ya sheria na kamati ya utendaji watafanya kazi na kama watakuwa wamefuata taratibu inaweza isifike huko kwenye CAF na FIFA,” alisisitiza Mwesigwa.
Mwesigwa alisema TFF itaendelea kuwasiliana na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit au Mwenyekiti, Yussuf Manji kwa mambo yote yanayohusu sera na mipango na siyo Bodi ya Wadhamini kama ambavyo Baraka alielekeza.
KUHUSU SIMBA SC
Mwesigwa alisema, katika mawasiliano ya barua ya Agosti 30, 2016 Simba walitoa majibu ya kuwa tayari wako kufanya hivyo wakati wowote wakihitajika na kuna wakati walikosa muda kwa sababu ya shughuli zao mbalimbali za klabu.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment