“Mi naona walikosa umakini, lakini kukosea ni kitu cha kawaida, as long as waligundua wamekosea na wakafanya kitu sahihi sio kama kuna tatizo,” Nick alimwambia mtangazaji wa kipindi cha The Vibe cha Mashujaa FM ya Lindi, Baby Dinny.
Nick amedai kuwa kosa walilolifanya limeonesha kuwa wao ambao wanatazamiwa kuwa na umakini wa hali ya juu nao hukosea.
Kurudishwa kwa tuzo hiyo kwa Alikiba kulipokelewa kwa furaha kubwa japo mambo yaligeuka kuwa mabaya baada ya watu kuanza kumtukana Wizkid. Hali hiyo ilimlazimu Alikiba kuwaomba watu wasiendelee kufanya hivyo na kudai kuwa mashabiki wake hawawezi kufanya hivyo.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment