Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii Ikulu jijini Dar es salaam, Magufuli alisema alitamani kuhudhuria tamasha hilo ili apige tumba lakini majukumu ya kazi yamembana.
“Natamani kwenda Fiesta siku ya kesho sema hii kazi inanibana kwa kuwa itakuwa live nitaifuatilia kupitia kwenye runinga,” alisema Magufuli.
Pia Rais huyo ambaye kesho November 5 anatimiza mwaka mmoja toka aingie madakani, alimmwagia sifa msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto kwa kufanya muziki wenye maadili na kuelimisha.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment