Nov 9, 2016

Wabunge Waigomea Serikali, Wakataa Kupangiwa Mishahara, Posho na Marupurupu

Wabunge  wamegomea hatua ya Serikali kutaka kusimamia posho na marupurupu yao, huku wakitaka suala hilo waendelee kujipangia wenyewe.

Msimamo huo uliotolewa na Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, umetolewa  baada ya Serikali kuwasilishwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba tatu ya mwaka 2016.

Awali Serikali ilitaka suala la stahiki hizo kwa watumishi wa umma liamuliwe na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora.

Akisoma maoni ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohammed Mchengerwa, alisema wametoa pendekezo hilo katika  Sheria ya Utumishi wa Umma sura 298    kulinda dhana  ya mgawanyo wa madaraka.

“Tume ya Utumishi wa Bunge na Tume ya Utumishi wa Mahakama zipewe uhuru  kusimamia upangaji wa mishahara, posho na marupurupu mengine,” alisema.

Akizungumzia mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, alisema kifungu cha 18 cha Muswada huo kuhusu muda wa mnufaika   kurejesha mkopo, Mchengerwa alisema kamati inashauri mkopo uwe mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo.

Alisema hali hiyo itasaidia kutoa fursa kwa mnufaika kuanza kulipa mkopo wake,   utaratibu ambao hutumika katika nchi nyingine kama Kenya na Zambia.

“Kuhusu wanufaika waliojiajiri kamati inapendekeza kiwango cha kurejesha mkopo kisipungue Sh 100,000 badala ya Sh 120,000 kama Serikali ilivyopendekeza,” alisema Mchengerwa.

Awali, akiwasilisha hotuba ya mabadiliko ya sheria hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, alisema   kifungu cha 8 cha Sheria hiyo kinaanisha mamlaka ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (Utumishi) kuwa ni pamoja na kufanya uchunguzi kwa ajili ya kuendeleza ufanisi wa utumishi wa umma.

Alisema Ibara 24 ya Muswada huo inapendekeza kuongeza kifungu kipya cha 9A cha Sheria kinachoweka masharti kuwa Taasisi, Wakala au Tume za Serikali hazitakuwa na mamlaka ya kuidhinisha mishahara na marupurupu kwa watumishi wa taasisi hizo na badala yake kibali kwa ajili hiyo kitatolewa na Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais (Utumishi).

“Marekebisho hayo yanalenga kuwa na mamlaka moja inayoratibu mishahara, posho na marupurupu na watumishi katika taasisi za Serikali na pia kuwianisha mishahara posho na marupurupu mengine kwa watumishi wa taasisi hizo.

“Masharti yaliyopendekezwa hayatatumika. Ibara hiyo imefutwa na kuandikwa upya masharti yanayopendekezwa hayatatumika kwa mishahara, marupurupu na masilahi mengine kwa Bunge,Mahakama, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Polisi,Magereza,JKT, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Usalama wa Taifa ili utaratibu huo kuendelea kama ilivyo sasa katika sheria zinazosimamia taasisi hizo.

“Kifungu cha 20 (1) (c) cha Sheria ya Utumishi wa umma kinaipa Tume ya Utumishi wa Umma mamlaka ya kutunga kanuni kuhusu usaili wa watumishi wa umma unaofanywa na tume hiyo,” alisema Masaju

Awali kifungu cha 8 kilikuwa kinapendekeza kufanyiwa  marekebisho  kumpa mamlaka Katibu Mkuu (Utumishi) kurekebisha na kuwianisha  mishahara, posho na marupurupu mengine kwa watumishi wa umma wakiwamo   wabunge na idara ya mahakama.

Huku ikipendekeza kuongeza kifungu kipya cha 9A kinachozizuia taasisi za umma, wakala, bodi na tume zisirekebishe au kuwianisha mishahara, posho na marupurupu mengine  kwa watumishi.

Sehemu ya tano inapendekeza marekebisho katika Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 kwa lengo la kutoa tafsiri ya neno “recruitment secretariat”, maneno hayo yametumika katika Sheria lakini hayakuwa yamepewa tafsiri.

Kiama kwa waajiri
Alisema Ibara ya 19 ya Muswada huo, inapendekeza kufuta kifungu cha 20 na 21,ambacho kilikuwa kinaeleza kwa kuwa si rahisi mwajiri kufahamu kama mtumishi anayeajiriwa ni mnufaika wa mkopo.

Kutokana na hali hiyo,alisema Muswada unaainisha kuwa mwajiri atatakiwa kuifahamisha Bodi ya Mikopo ndani ya siku 28,baada ya mwajiriwa huyo mwenye Shahada au Astashahada ili bodi  iangalie kama mwajiriwa huyo ni mnufaika wa mikopo.

“Mwajiri ambaye atashindwa kutekeleza masharti ya kifungu hicho atakuwa anatenda kosa la jinai ambalo adhabu yake ni Sh milioni moja au kifungo cha miezi sita gerezani. Pia inapendekezwa baada ya mnufaika wa mkopo mwajiri atatakiwa kukata asilimia 15 ya mshahara wa mwajiriwa.

“Bodi au mawakala wake wawe na mamlaka ya kukagua kumbukumbuku za waajiriwa kwa lengo la kufuta taarifa zinazohusiana na wanufaika wa mkopo pamoja na kumbukumbu za  waajiriwa kwa lengo la kutafuta taarifa zinazohusiana na wanufaika wa mkopo kwa hatua zao muhimu kuhusu makusanyo wa mikopo,” alisema

AG Masaju alisema kifungu cha 57 cha sheria hiyo, kinaweka masharti kuhusu zuio kwa shughuli za binadamu zinzoathiri ulinzi wa bahari, mito, mabwawa zisifanyike ndani ya mita 60 kutoka kingo za bahari, mito au mabwawa.

Alisema hatua hiyo imekusudiwa kuimarisha ulinzi na usalama wa mazingira ya maeneo husika ya bahari, maziwa na mito na mabwawa.

“Ibara ya 11 ya Muswada inapendekeza kifungu hicho kirekebishwe katika kifungu kidogo cha pili   kuweka mwongozo wa namna ya kupima mita 60 ambako shughuli za  binadamu zimezuiliwa kufanyika.

“Kifungu cha 184 kinaeleza athari na uthamini wa mazingira. Ibara ya 12 inapendekeza kuwa kitendo cha mtu yeyote kushindwa au kukataa kufanya tathimini ya athari za Mazingira kwa mradi unaohitaji tathmini hiyo kufanyika ni kosa la jinai ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua Sh milioni tano na isiyozidi Sh bilioni moja au kifungo kisichopungua miaka miwili,” alisema.


Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger