Kesi hiyo imesikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ambapo upande wa mshtaki amedai kuwa Novemba 20 mwaka jana alimkopesha mdaiwa TZS milioni 80 kwa makubaliano ya kulipa fedha hizo katika kipindi walichokubaliana lakini hajafanya hivyo.
Mdai alisema kuwa Mei 22 mwaka huu alipewa kiasi cha TZS milioni 5 na fedha nyingine zilizobaki (TZS milioni 75) hajapewa hadi leo.
Hakimu Is Haq Kuppa aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena huku upande wa wadaiwa wakiomba siku sita kuweza kujibu tuhuma hizo.
Wakati hayo yote yakiendelea mdaiwa, Hussein Mkangala hakuwepo mahakamani.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment