Akizungumzia tukio hilo leo Mkoani Singida Waziri Mwigulu amesema kitendo cha kukutwa kwa wahamiaji zaidi ya 80 wakiwa na majeraha na hawajiwezi mkoani Pwani kinahusisha kwa namna au nyingine na maiti zilizookotwa mto Ruvu
Waziri Mwigulu amesema kuwa watu hao ambao wamezikwa na serikali licha ya ndugu au taifa lolote kujitokeza sheria inawaruhusu kufanya hivyo kutokana na kutokutambulika kwa watu hao.
Mhe. Mwigulu amesema bado wanaendelea na uchunguzi juu ya matukio hayo ikiwa na operesheni mbalimbali za kutokomeza matukio ya kihalifu pamoja na wahamiaji haramu nchini
Serikali imeiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani kuhakikisha wanawakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria watu waliowaua watu saba waliokutwa kandokando ya Mto Ruvu.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment