Hakuna kiongozi wa ccm atakuja asianze sifiwa sana mwanzo, muda mfupi baadae. Kilio Cha hujuma toka ndani kisianze, kisipoanza cha hujuma basi watendaji wake wataambiwa ndio hawana sifa, baadae wanarudi tena ktk hujuma. Hii ni pattern inayojirudia. Ni pattern hihi inayoweza onekana kwa watu wasio na utaratibu wa maisha, au wanaomini mifumo, imani, na mila zilizoshindwa ktk dunia ya wakat huo.
Ni CCM hi hi imejengwa ktk ujamaa unaominisha watu unaoaminisha watu kwamba kushindwa kwao kunatokana na watu fulani wanaitwa mabeberu na si mipango na uendeshaji mbovu wa maisha yao.
Sitegemei popote katika maisha haya utawala huu mpya utakapoona mambo hayaendei wakimbilie ktk hoja kwamba anahujumiwa. Itakuwa ni kipindi km taifa kujiuliza km tunahitaji tena ccm ili tutoke ktk hii vicious cycle.
Tutakaposikia hii kilio cha kuhujumiwa basi wajue sisi wananchi ndio tuna kila sababu ya kuhujumiwa na tutahitaji nasi kulia hicho kilio na kudai fidia ya hizo hujuma.bado hatujalia, kwa vile tunaamini kulalama sio tiba, ila kuwakumbusha kwamba shida ni mfumo uliopitwa na wakati unaoshikiliwa na uwepo na chama kilichopitwa na wakati.
Ccm na hii nchi ni kama mdudu au binadamu aliyeingiwa ktk jiji na akitafuta njia ya kutoka huku akitembea kwa miguu,huku mitaa mingi ikizunguka hapo hapo na mingine haichomozi. Wapinzani ni km watu waliopo ktk jiji hilo hilo huku wakiwa na gari na chopa pamoja na google map. Ukiwa na chopa unaona mitaa na unaweza mwongoza mtembea kwa miguu mitaa ipi inachomoza. Ccm ni mtembea kwa miguu mpuuzi anayebishana na mwenye kujua njia huku akiwa hana njia ya kutoka. Mwishowe anaishia kurudi palepale
Magufuli akitaka fanikiwa hana haja ya kupoteza muda na kazi ngumu yenye tija ndogo kwa kujenga nyumba juu ya msingi wa mchanga mtupu CCM.
Anachoweza fanya cha kukumbukwa ni kuibomoa kabisa CCM. Mengine yatajiendesha yenyewe. Nchi nyingi zenye mifumo mizuri hujiendesha zenyewe. Ccm imetengeneza nchi hata ikiwa na uongozi haiendi sana. Ccm ni kikwazo kikubwa sana.
Ujamaa ni km mganga anayetambika wengine wapate pesa, huku yeye akipewa kidogo zaidi. Kwa misemo ya CCM mganga hajigangi. AS If mganga hawezi kunywa dawa anayompa mtu. Hamjawahi sikia watu wote waliojifunza vitu kwetu wamekwenda pata tuzo? SABABU Ni nini? Ni kwamba mchawi hastahili chochote ktk hii, mchawi ni km mtumwa anayeshikia vitu watu hadi wenyewe(warithi) waje chukua. Mwishowe hujisifu kwamba wao ndio watoa risiki, wao ndio watoto wa mjini, wao ndio master planners.
Kwa aliyewahi sikia huu usemi.."ULE Mradi ulikuwa mzuri sana hadi zilipoingia siasa" kwa lugha nyingine hawakusema tuu "ilikuwa nzuri hadi ilipoingia CCM". Walipogusa tuu ikanajisika.
Ujamaa si kitu halisia. Wajamaa kila ktk maonyesho yao ni uongo na kinaishia kuwa maonyesho tuu na si kwa matumizi. NI Kujionyesha tuu kuwa nao wapo au zaidi ila si vitu halisi. Kwa miaka yote tz ktk maonyesho utaona sample nyingi .
HATA Kilimo siku zote ni nursery.Hata kelele za kilimo kwanza ni maonyesho tuu.. WANAOFANYA Serious ni wale waliokuja ktk maonyesho. Dunia nzima kuna nchi zilijifunza kilimo kwanza na sasa wanakata mbuga. Wanachoweza ni kukwamisha wazawa kwa vile ndio size yao, ndio namna ya kuendesha huu mfumo ulioumbwa na wivu ndani yake, mfumo wenye ghiliba na kuchukia mafanikio. Waliofanikiwa kuharamishwa.
Kwa bahati mbaya sana watu hawajaona . Ila nadhani watz wacha mungu wangekuwa wamefunguka kidogo "wangefanya maombi ya kumshukuru mungu kwamba tupo salama hadi sasa". Mpaka sasa ujamaa na jiko lake CCM wameshafikisha watz ktk stage ya mbali sana kugeuzwa magaidi. Watz walipewa adui, wakapewa sababu za kuchukia, wakapewa moyo na nia ya kupigana, wakapewa kinga wasipate kuamka akili(wakaambia kila anayeamsha ni kibaraka asiyetakia nchi mema, kuwa anayewaamsha anataka madaraka). KISHA Wakapoozwa kusubiri amri ya uongozi mkuu..
PROPAGANDA Machines zote kuanzia vyuoni, mabalozi, na waandishi wote kazi ni moja kuwageuza magaidi na kuwakinga na wokovu. Ukiwasikiliza watz ktk mijadala unaweza tapika jinsi wanavyoongea km misukule bila aibu. Hata Walioona mwanga hawakuweza ona vyema kwani tayari matongotongo na ukungu yalishaganda sana machoni. Mara nyingine wakingalia vitu wanakuwa na wasiwasi km ni chenyewe.
Magufuli pole sana, hiyo ndio CCM na watu wake na uwezo wao. Makosa mengine si hujuma ndivyo akili zao zinawatuma kwamba wanafanya best thing around for the party. Ni makada walioapa kufia chama na mwenyekiti wake.
Soon utakuwa mwenyekiti utapewa utiifu wa kutisha. Hata yule mama shem wako kwa wajina alikuwa anatimiza wajibu wake kwa chama. Kutetea chama ili hayo mambo ya wezi wa mishahara kwa watumishi hewa mkamalize sirini km munge la siri.
Ndio akili za kijamaa, na bahati mbaya sana wajamaa huwa issue zao zinajigonga pabaya sana kiasi cha kuwafanya wasiamini km treni zao ni km nyumba ya babel na hakuna mkono wa mtu. Ujamaa ni shetani ndio maana wanajipa uungu kwamba binadamu(mwananchi ana mapungufu sana bila kuongozwa na kusaidiwa fikiri atatumbukia shimoni).
Wajamaa kwa vile miungu, chama ni dini, ikulu ni mbingu na mwenyekiti ndio mwenye fikra pekee sahihi. Basi huwasaidia wananchi kuchagua habari takatifu ili yule mwovu asiyewazidi. Basi Nape malaika mlinzi kaamua kuwasaidia wananchi wasisikie akina Kitwanga na akina Lema waovu wakubwa wanaoleta vitu vya kutwanga. Na kumvuta mungu(aka mwenyekiti sharubu).
Imagine Cuba leo ndio inapata internet na tv kwa wananchi wake. Pamoja na elimu na uwezo wa watu wake.Leo Cuba km gereji kubwa ya kukusanyia magari ya kizamani. WANGEKUWA Si wajamaa leo wangekuwa wapi?
Sidhani km Marekani ndio waliwanyima Cuba kuwa na internet zaidi ya Mungu Castro mlezi wa kila raia, mungu wao na baba yao wa kulinda hadi na fikra mpya.
Huo ndio ujamaa km ugaidi ulivyoacha nchi za watu na mateso makubwa bado wanaamini wengine ndio wanawahujumu km vile wengine ndio waliwalisha hizo itikadi za kuwazungusha ktk matatizo bila kutoka.
In fact kilio chochote cha utawala huu kuhusu kuhujumiwa ni ushahidi tosha kwamba shida si kiongozi ni CCM(mfumo usio na mpangilio wenye maana). MAGUFULI Alijibainisha km CCM na serikali akaiita yake. Watz wakaamini km ni yeye basi nchi itakwenda. Sasa hata yeye anaona CCM ndio shida. Wapinzani walikuwa sahihi.
Oto za kifikra na nawasilisha rasmi.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment