Hiyo ni siku chache tangu Aveva ataje sababu ya timu hiyo kukosa ubingwa huo uliochukuliwa na Yanga.
Beki huyo, tayari amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga kwa dau la shilingi milioni 40 huku akilipwa mshahara wa shilingi milioni 2 kwa mwezi.
Kessy alisema alichokifanya rais huyo ni kumtumia kama mwamvuli kuwafunika viongozi hao ili wasionekane kikwazo cha wao kushindwa kuiwezesha timu hiyo kutwaa taji hilo.
Kessy alisema kwanza kabisa aliondoka Simba ikiwa timu hiyo imebakiza michezo mingi ambayo kama viongozi na benchi la ufundi wangefanya kazi yake vizuri, ingechukua taji hilo, hivyo anashangaa yeye kutajwa.
Aliongeza kuwa, viongozi hao wasiitumie njia hiyo kumharibia kwa baadhi ya mashabiki wa timu hiyo huku akipanga kwenda kuwavaa mabosi hao akidai malipo yake ya mshahara wa mwezi uliopita baada ya kupata taarifa za malipo hayo.
“Kwanza hao viongozi wa Simba wasijisahaulishe kabisa, wakumbuke ninawadai malipo yangu ya mshahara wa mwezi uliopita, tayari nimeshamwambia katibu wao ninataka mshahara wangu"
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment