Mkaguzi wa Dawati la Jinsia katika kituo cha Polisi Oysterbay Bi. Prisca Komba amesema vitendo vya ukatili wa jinsia nchini bado vipo kwa kiasi kikubwa hasa kwa upande wa vijana waliopo kwenye mahusiano.
Bi. Komba ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu na East Africa Radio na kusema kuwa katika kuhakikisha wanapambana na matatizo ya ukatili wa kijinsia nchini wameanza kushirikiana na wadau mbalimbali wa taasisi za umma na binafsi katika kuhakikisha wanalipinga tatizo hilo ndani ya jamii zetu.
Amesema ndoa nyingi za vijana kwa sasa zimekua hatarini kwakuwa tayari vijana wamejikita katika vitendo vya starehe na mikusanyiko mikubwa ya kuwashawishi kuingia na kufanya starehe hivyo kuwafanya vijana wengi kusahau kuhudumia familia zao.
Amesema bado wanakumbana na changamoto ya vijana na jamii kutokua wawazi kwa kuwafichua waalifu wa vitendo hivyo na wengine wanayamaliza matatizo hayo kwa njia ya kifamilia ambayo sio sahihi ndani ya jamii na kupelekea vitendo hivyo kuendelee kutokea.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment