May 16, 2016

Serikali Yafufua Kesi ya Zombe Kivingine

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amemuondolea kosa la mauaji  aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na sasa inataka ajibu mashtaka ya kuficha wahalifu.

DPP amefanya mabadiliko hayo kwenye rufaa aliyoikata Mahakama ya Rufani dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumuachia huru Zombe, ambaye alikuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) katika mashtaka ya mauaji.

Awali, DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachia huru Zombe na wenzake tisa, katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva mmoja wa teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam.

Katika rufaa hiyo, DPP alikuwa anaiomba Mahakama ya Rufani iwatie hatiani washtakiwa hao kwa kosa la mauaji ya kukusudia, kama ilivyokuwa kwenye kesi ya msingi, kosa ambalo adhabu zake ni pamoja na kunyongwa hadi kufa.

Hata hivyo, DPP amebadili msimamo huo dhidi ya Zombe na badala yake anaiomba Mahakama hiyo imtie hatiani kwa kosa la kuwalinda wahalifu ambao walitenda kosa la mauaji ya wafanyabiashara hao na dereva wa teksi.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti, Timoth Vitalis, ambaye ni Wakili Mkuu wa Serikali (PSA) na Richard Rweyongeza, ambaye ni wakili wa kujitegemea anayemtetea Zombe katika rufaa hiyo, walisema mtu anayepatikana na hatia kwa kosa hilo adhabu yake ni kifungo jela kisichozidi miaka saba.

Kwa maana hiyo, hata kama Mahakama ya Rufani itakubaliana na hoja za rufaa za DPP na kumtia hatiani Zombe kwa kosa hilo jipya ambalo hata hivyo, hakuwa ameshtakiwa nalo kwenye kesi ya msingi, atakuwa ameepuka adhabu ya kitanzi.

DPP alibadili msimamo wake huo dhidi ya Zombe siku ya usikilizwaji wa rufaa hiyo Mahakama ya Rufani mbele ya jopo la majaji watatu, Bernard Luanda, Sauda Mjasiri na Semistocles Kaijage, hivi karibuni.

Mkurugenzi huyo wa mashtaka alifikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani Zombe kwa kosa hilo la mauaji.

Akizungumzia uamuzi huo wa DPP kumuondoa kwenye shtaka la mauaji kama alivyokuwa akidaiwa tangu awali na sasa kupewa shtaka la kuwalinda wahalifu, Zombe alisema kwanza alikuwa ameonewa kwa kuhusishwa na hatimaye kushtakiwa kwa kosa la mauaji.

Alisisitiza kuwa hakutendewa haki wakati wa kumfungulia shtaka hilo la mauaji  kwa kuwa sheria hazikufuatwa.

“Kwanza ni mambo ya ajabu sana. Nimedhalilishwa sana kwa muda wote huo na kuonekana kuwa mimi ni muuaji kila ninakopita, kwa kufunguliwa shtaka ambalo sikuhusika nalo,” alisema Zombe.

“Mimi sikuwapo eneo la tukio na wala nilikuwa siwafahamu watu hao na hata Tume (iliyoundwa na Rais kuchunguza mauaji hayo iliyoongozwa na Jaji Mussa) Kipenka ililiridhika kuwa sikuwepo eneo la tukio. Sasa nilihusikaje na mauaji hayo?”

Zombe aliongeza kuwa washtakiwa wote walihojiwa na kuandika maelezo yao na kwamba huo ndiyo utarartibu wa kisheria.

Zombe alisisitiza kuwa yeye alikuwa mwendesha mashtaka kwa muda mrefu na mkuu wa upelelezi wa mkoa, hivyo anajua taratibu kwa kuwa alikuwa akiandika majalada mengi kwenda kwa Mwanasheria wa Serikali na mengine yalikuwa yakienda mahakamani kama alivyoyaandika.

Kuhusu kosa alilobadilishiwa na DPP wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, Zombe hakuwa tayari kulizungumzia kwa kuwa bado Mahakama haijatoa hukumu.

 Kabla ya kumbadilishia shtaka hilo, wakati wa usikilizwaji wa rufaa, DPP alitaka kumuongezea Zombe shtaka hilo kama shtaka mbadala, wakati wa usikilizwaji wa kesi ya msingi.

 Hata hivyo, DPP aligonga mwamba baada ya Jaji Massati kumkatalia kwa maelezo kuwa alitakiwa ashtakiwe tangu mwanzo kwa kosa hilo.

Kabla ya kumuondoa Zombe katika kosa la adhabu hiyo ya kunyongwa, kwanza DPP, aliwaondolea washtakiwa wengine watano, baada ya kubaini kuwa ushahidi aliokuwa nao hauwagusi katika rufaa hiyo.

Walioondolewa ni Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Abineth Salo na Festus Gwabisabi.

Lakini ameendelea kuwang’ang’ania Zombe na wenzake watatu ambao ni Christopher Bageni, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.




Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger