May 9, 2016

Ukawa: Hii Sasa Dharau

MGONGANO wa kiutawala umeanza kufukuta katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam, anaandika Happiness Lidwino.

Charles Kuyeko, meya wa manispaa hiyo ameeleza kwamba, hayuko tayari kuona viongozi wanaotokana na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanakiuka mipaka ya taratibu za kazi kwa sababu za kiitikati ama dharau.

Meya huyo anayetokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) amesema, hatua ya Isaya Mgurumi, mkurugenzi wa halmashauri hiyo alilotoa juzu kuwatimua wafanyabiashara wamachinga mjini bila kufuata taratubu inaonesha dharau.
Amesema, Mgurumi amefanya hivyo bila kumuhusisha meya na madiwani wa manispaa hiyo. Kutokana na kutishirikishwa kwao, leo wametengua uamuzi wa mkurugenzi huyo.

Katika kikao cha dharura kilichoitishwa leo na meya huyo, madiwani wa CCM hawakuhudhuria ambapo waliohudhuria ni madiwani kutoka kwa vyama upinzani.

Madiwani hao wamewataka wamachinga kutoondoka katika maeneo yao hadi watakapotafutiwa maeneo manzuri ya kufanyia biashara, huku wakimtaka mkurugenzi kurudi mezani kwa ajili ya mazungumzo.

Mgurumi juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, aliwataka wamachinga waliopo maeneo ya mjini hususan barabarani kuondoka mara moja ndani ya siku tatu.
Pia aliwapangia maeneo ya kwenda kufanyabiashara zao ambayo ni Ukonga Magereza, Muslimu Tabata, Kigogo Fresh na Kivule huku akiwatisha kwamba, atakayekaidi  tamko hilo, mgambo na askari wa mabomu watafanya kazi yake.

Akizungumza na waandishi leo ofisini kwake Kuyeko amesema, amesikitishwa na tamko hilo ambalo hakushirikishwa kama kiongozi wa manispaa hiyo.

Amesema, badala ya kushirikishwa, aliletewa tamko hilo ili kutolea msisitizo.
“Nashindwa kuwaelewa viongozi wenzetu kwa kushindwa kutushirikisha masuala ya maendeleo katika manispaa tunayoiongoza wote.

“Yaani baada ya kufanya uamuzi na Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa basi sisi wengine ambao tupo kwa niaba ya wananchi tunaonekana hatuna maana tena.
“Baada ya kutoa tamko ndio naambiwa nitoe msisitizo, hiyo ni dharau na ndio maana sikufanya hivyo,” amesema Kuyeko.

Amesema, licha ya yeye kutopewa taarifa hata madiwani wa maeneo ambayo mkurugenzi amewataka wamachinga kwenda hawana taarifa juu ya ugeni huo na kwamba, maeneo ya masoko hayatoshi kubeba watu wengi.

Patrick Assenga, Diwani wa Kata ya Tabata anasema, ameshangazwa na hatua mkurugenzi kufanya uamuzi kabla ya kuzungumza na viongozi wa maeneo husika.
“Hapa katika kata yangu soko halina vyoo wala maji ya kutosha, hata hivyo eneo ni finyu kutokana na kuwepo kwa shughuli nyingi za CCM ikiwepo ofisi yake na maegesho ya magari yao ambapo tumepiga kelele kwa muda mrefu waondoe shughuli zao lakini hadi sasa wamekaidi halafu wanaleta habari hizi,” amesema.

Stevene, Msigwa Mwenyekiti wa Wamachinga Wilaya ya Ilala amesema kuwa, wafanyabiashara hawana imani tena na serikali kwa kuwa, licha ya kushirikiana katika mambo mengi lakini imeamua kuwachukulia hatua kwa vitisho pasipo kuwashirikisha kwenye uamuzi huo.
“Ni vema wangetuita tufanye mazungumzo kabla ya kutuchukulia hatua kwani sisi ni binadamu na tuna majukumu, kuhamisha biashara kunahitaji maandalizi.

“Hatukaidi kuondoka ila hatutaondoka hata watumie mabomu hadi pale watakapotupatia maeneo manzuri yenye miundombinu mizuri kwani tunalipa kodi zetu,” amesema Msigwa.
Hata hivyo, madiwani waliohudhulia kikao hicho cha dharura wamesema, hawaina imani tena na mkurugenzi kutokana na maamuzi yake yasiyo shirikishi ambayo yanaonekana kuwa na shinikizo kutoka kwa Makonda.

Pia wamesema, endapo kesho shughuli hiyo itaendelea, watachukua hatua kali kutokana na kutosikilizwa.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger