Licha ya Mamlaka husika inayoshughulikia Mabasi hayo kuweka utaratibu maalum wa kuvuka na kuwataka wananachi kutotumia barabara hizo kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine, utaratibu ambao umekuwa mgumu kufuatwa..
Channel ten ilifika katika kituo cha mabasi ya mwendo kasi kilichopo kimara jijini Dar es salaam na kushuhudia watu mbalimbali wakivuka kupitia barabara ya mwendo kasi huku wachache wakitumia daraja lililowekwa na UDARAT ambapo katika mahojiano na Channel ten wananachi hao wamedai kuwa licha ya kufahamu kuwa utumiaji wa barabara hizo kunahatarisha usalama wao lakini wanavuka barabara hizo ili kurahisisha uvukaji kutokana na madaraja yaliyowekwa kuwa na mzunguko mrefu ambao baadhi ya watu wakiwemo walemavu na wazee kushindwa kutumia madaraja hayo.
Hali ya Usafiri wa mabasi ya mwendo kasi imezidi kuimarika tangu kuanza kwa huduma hiyo licha ya changamoto mbalimbali ambazo mamlaka husika tayari zimeahidi kuzishughulikia.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment