Sep 16, 2016

UVCCM Arusha Hapakaliki , Wazichapa Ngumi Kavu Kavu


Jeshi la Polisi mkoani Arusha jana asubuhi  lilituliza vurugu za viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya CCM (UVCCM) mkoani hapa, waliokuwa wakigombea ofisi. 

Vurugu hizo ziliibuka hadharani jana baada ya kuwapo taarifa za mgogoro wa chini kwa chini uliodumu kwa kwa miezi miwili, kati ya makundi mawili yanayokinzana kiuongozi. 

Mgogoro huo ulielezwa kukolezwa na uhamisho wa Katibu wa UVCCM Mkoa, Ezekiel Mollel kwenda makao makuu, huku katibu mpya aliyepelekwa kuchukua nafasi hiyo akikwama kukabidhiwa kwa siku tatu sasa. 

Katibu huyo mpya Saidi Goha, jana alitaka kuingia ofisini lakini alikumbana na kigingi cha kundi linalomuunga mkono Mollel lililofunga mlango kwa mnyororo. Kutokana na vurugu za jana, polisi wanamshikilia mwenyekiti wa miradi ya jumuiya hiyo, Phillemon Ammo pamoja  na  Mollel. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema: “Ni kweli tumemkamata lakini nina ugeni wa Serikali (wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan), naomba nitoe taarifa baadaye,” alisema Mkumbo. 

Lengai Ole Sabaya, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Arusha,  alisema anapinga na kulaani kitendo cha baadhi ya wanachama wa umoja huo kufunga ofisi hizo kinyume na taratibu. 

Mollel anadai  uhamisho wake ni njama za kupoteza ushahidi wa baadhi ya tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya fedha kwenye jumuiya hiyo, hivyo hatokwenda popote.

Anasema yeye anatekeleza maagizo ya kamati ya utekelezaji ya kusimamia mali za chama, kwani katika kipindi cha miezi miwili ameokoa zaidi ya Sh30 milioni ambazo zilikuwa zinaingia mifukoni mwa watu wachache.

“Tuna maduka hapa, waliopangishwa wanalipa zaidi ya Sh300,000 lakini chama kinapata chini ya Sh50,000 kwa duka kama kodi ya mwezi sasa tumetaka wenye maduka kulipa moja kwa moja UVCCM na siyo kwa watu wa kati na hapa ndipo chanzo cha mgogoro,” alisema. 

Kutokana na vurugu hizo zilizoibuka jana asubuhi,  Sekretarieti ya UVCCM imeamua kumsimamisha kazi bwana  Ezekiel Mollel. 

Kaimu Katibu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alitangaza uamuzi huo jana jioni muda mfupi baada ya Mollel  kukabidhi ofisi kwa katibu mpya wa UVCCM mkoa, Saidi Goha ambaye amehamishiwa Arusha akitokea Lindi, akiwa chini ya ulinzi wa polisi. 

Baada ya makabidhiano hayo polisi walimrejesha kituo kikuu cha polisi anakoshikiliwa. Shaka alisema, Mollel aliandikiwa barua ya uhamisho kwenda makao makuu tangu Agosti 25, na alitakiwa kukabidhi ofisi ndani ya siku 14 lakini aligoma. 

Alisema Mollel amekiuka kanuni za utumishi za UVCCM, hivyo Baraza Kuu na Kamati ya Utekelezaji Taifa watatoa uamuzi zaidi kwa mujibu wa kanuni kwa kuwa ukomo wa sekretarieti ni kumsimamisha. 

Hata hivyo, Mollel akizungumza akiwa chini ya ulinzi, alisema makabidhiano hayo ni batili kwa kuwa hakuyasaini.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger