Wanaojiita wafuasi wa Lipumba wamesema hawatamruhusu Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Shariff Hamadi na baraza lake kuingia katika ofisi za chama hicho hadi atakapo kubali kumtambua Lipumba kama mwenyekiti wake.
Taarifa ya kuaghirishwa kuwasili baraza hilo ilitolewa jana usiku na Kiongozi wa wabunge wa CUF bara, Riziki Ngwale ambapo aliwataka wanachama na wabunge wasiende katika ofisi hizo kutokana kwamba walifanya utafiti na kubaini kuwa kuna wanajeshi wanao mlinda Lipumba.
Hadi muda huu, wafuasi wa Lipumba wamezingira geti kuu la kuingilia wakisubiri viongozi wa baraza hilo kama watawasili.
Mmoja kati ya wafuasi hao ambaye hakutaka kutaja jina lake, ameuambia mtandao huu kuwa, hawataruhusu baraza hilo kuingia hadi watakapo mkubali Lipumba.
Na pia amesema viongozi wote waliosimamishwa uanachama watarejea katika nafasi zao za awali akiwemo Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF, Abdul Kambaya na Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya.
Aidha, Lipumba anatarajiwa kuongea na waandishi wa habari wakati wowote kuanzia sasa, na kwamba yupo katika ofisi yake hadi muda huu.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment