Nov 14, 2016

Kesi ya Akina Zombe: Mrakibu wa Polisi (SP) Bageni Apinga Hukumu ya Kunyongwa Hadi Kufa

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Mrakibu wa Polisi (SP),Christopher Bageni amewasilisha maombi Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kupinga adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

SP Bageni alihukumiwa adhabu hiyo baada ya mahakama hiyo kujiridhisha kwamba aliwaua kwa kukusudia wafanyabiashara wanne wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva teksi mkazi wa Manzese, Dar es Salaam,  katika Msitu wa Pande.

Bageni kupitia Wakili wake, Gaudioz Ishengoma,  aliwasilisha maombi hayo mwishoni mwa wiki yaliyoambatana na hati ya kiapo iliyoapwa na wakili huyo.

Muwasilisha maombi anaomba mahakama hiyo kuifanyia marejeo hukumu dhidi yake iliyotolewa Septemba 13 na kusomwa  Septemba 16 mwaka huu na Msajili wa Mahakama hiyo, John Kahyoza.

Akitoa sababu kuomba marejeo, anadai  alinyimwa haki sawa ya kusikilizwa wakati wa kutathmini ushahidi ulioko kwenye kumbukumbu za mahakama kwa kuegemea kwenye ushahidi wa upande wa mashtaka.

Alidai katika kuchanganua ushahidi ambao uamuzi wa mahakama uliegemea, mahakama ilishughulika na ushahidi wa msingi (Exam in Chief) wa upande wa mashtaka na iliangalia kwa juu juu tu ushahidi wa utetezi hususan wa Bageni au haikuutazama kabisa.

“Kuna kukinzana kwa haki kwa maana ya kwamba mtoa maombi alinyimwa haki sawa ya kusikilizwa, kwa mahakama kuchagua na kuegemea   upande wa mashtaka pekee na kushindwa kuzingatia ushahidi wa upande wa utetezi, hasa wa mtoa maombi.

“Uamuzi wa mahakama umetolewa katika msingi wa makosa ya dhahiri kwenye kumbukumbu za mahakama, hivyo kusababisha upotoshaji wa haki, kushindwa kuzingatia mwongozo wa kanuni katika asili, thamani na matumizi ya ushahidi wa kuungwa mkono,” ilisema sehemu ya maombi hayo.

Alidai kuwa kwa kushindwa kuchanganua na kutathmini  ushahidi kwa umakini kwenye kumbukumbu, mahakama ilishindwa kuainisha ushahidi wa mjibu rufaa wa nne (Bageni)  kimazingira kama ilivyo ni dhahiri unakosa thamani ya kuhitaji ushahidi wa kuunga mkono na hivyo si salama kuegemea katika kumtia hatiani.

“Kwa kushindwa kuona na kuzingatia ushahidi uliokusudiwa kuwa na ushahidi wa kuunga mkono, siyo ushahidi huru na hauna mashiko kuthibitishwa (PW27) na haupo (PW36).

“Kwa kushindwa kufanya uchambuzi wa ushahidi kwenye kumbukumbu kwa umakini wenye manufaa, vinginevyo mahakama ilipaswa kuona wajibu wa kuthibitisha shtaka kwenye jinai haukufikiwa,”anasema Wakili Ishengoma.

Anadai mahakama katika kuamua, kama ilivyofanya katika uhalisia wake, kuhusu ushiriki wa mtoa maombi katika eneo la tukio la uhalifu, ilishindwa kubaini katika ujumla wake ushahidi wa upande wa mashtaka ambao haukuweza kuthibitisha mashtaka bila kuacha shaka.

Ishengoma alidai mahakama haikuuchukulia ushahidi kwenye kumbukumbu katika ujumla wake hivyo kutengua uamuzi wa kuachiwa huru kwa mtoa maombi na kumtia hatiani na kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kusimamia ushahidi ambao haupo na uvumi pamoja na ushahidi wa mashaka makubwa.

Alidai kutokana na hukumu ya mahakama, haikuwa bayana ni kwa ushahidi wa nani ulithibisha mtoa maombi Bageni alimwezesha au kumsaidia nani katika mauaji ya marehemu hao.

Katika hati ya kiapo iliyoapwa na Wakili Ishengoma, Bageni anadai yeye na wengine wanane ambao hawako katika maombi hayo walishtakiwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa makosa ya mauaji ya watu wanne katika Kesi ya jinai namba 26 ya mwaka 2006.

Bageni alikuwa mshtakiwa wa pili na katika hukumu iliyotolewa na Jaji Salum Massati, amnayo  wote waliachiwa huru, lakini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hakuridhishwa na uamuzi huo hivyo alikata rufaa namba 358 ya mwaka 2013.

Kabla ya usikilizwaji wa rufaa hiyo, DPP aliwaondolea rufaa wajibu rufaa watano na kubaki wajibu rufani wanne ambao waliachiwa huru pia Septemba 16, mwaka huu.

Walioachiwa huru ni aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe na maofisa wengine wawili baada ya mahakama kuona hakuna ushahidi wa wazi ama mazingira kuwatia hatiani.

Katika kesi ya msingi, Bageni alidaiwa kuwaua kwa kukusudia wafanyabiashara Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na Juma Ndugu, aliyekuwa dereva wa teksi wa Manzese , Januari 14, mwaka 2006, katika Msitu wa Pande, Mbezi Luis, Dar es Salaam.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger