Nov 5, 2016

Mwaka Mmoja Wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Leo na mimi nipaze sauti yangu imfikie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa Mafanikio Makubwa aliyoyapata ktk kipindi cha Mwaka mmoja wa utawala wake tangu aingie madarakani mnano Novemba 05, 2015.

Rais Magufuli kwa kiasi kikubwa amerudisha nidhamu kwa watumishi wa umma. Leo ofisi nyingi za utumishi wa umma zina nidhamu ya hali ya juu sana, watu wanatambua vizuri nini wanapaswa kufanya na nini hawapaswi kufanya ktk Utumishi wao. Huduma zenye kukidhi matakwa ya wananchi zimerejea.

Rais Magufuli amefanikiwa  kwa kiasi kikubwa  kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali kwa kuzuia na kufuta matumizi yasiyokuwa ya lazima kama safari za nje ambapo ktk kila safari kwa sasa ni lazima Ikulu ibariki kwa kutoa Kibali na kuruhusu idadi ndogo tu ya watu na mara nyingine mabalozi kuiwakilisha Tanzania, kuondoa posho zisizo za lazima n.k

Rais Magufuli  alielekeza fedha mbalimbali ambazo zilitengwa kwa matumizi Maalum Mfano Fedha kwa ajili ya Semina kwa Baraza la Mawaziri, Fedha kwa ajili Sherehe ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Uhuru - 09 Desemba 2015 n.k  Mh. Rais alielekeza  zikafanye Shughuli za Kimaendeleo ikiwemo kununua Vitanda vya Hospitali ya Taifa Muhimbili na kutengeneza Madawati kwa ajili ya Shule za msingi  ili kuboresha Elimu.

Rais Magufuli alituahidi endapo atachaguliwa   Elimu ya msingi na Sekondari itakuwa ni BURE ambapo ametimiza sasa Elimu kwa Shule za Msingi na Sekondari ni BURE kabisa.

Rais Magufuli aliahidi atafufua Shirika la Serikali la Ndege la ATCL kwa kununua Ndege Mpya ambapo tayari Mheshimiwa Rais ametimiza Ahadi yake kwa Kununua Ndege Mbili Mpya  na leo ameahidi kutuletea Ndege Kubwa aina ya Boeing yenye uwezo wa Kubeba abiria zaidi ya 240 ili kukuza uchumi wa Nchi kupitia  Sekta ya Utalii.

Rais Magufuli amefanikiwa kusimamia ipasavyo Ukusanyaji wa Mapato ya serikali na Kudhibiti Matumizi yake. Hongera pia Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais ktk hili.

Rais Magufuli alituahidi kupambana na Ufisadi na Kuendeleza Vita dhidi ya Wala Rushwa kwa Kuanzisha Mahakama ya Kushughulikia Ufisadi na Rushwa na tayari mahakama ya Kushughulikia Ufisadi & Rushwa inaishi na leo naamini imesikiliza Kesi moja.

Rais Magufuli ameendelea kuboresha barabara kwa Kukijenga kwa Kiwango cha lami mfano kama ile ya Mwenge Dar es Salaam & Mwanza.

Mheshimiwa Rais aliahidi kuhamishia Serikali yake Makao Makuu ya Tanzania Mjini Dodoma na tayari amekwisha anza kutekeleza kwa kuhamisha Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara mbalimbali.

Rais Magufuli aliahidi kukuza Uchumi wa Nchi yetu kwa kuifanya Tanzania ya Viwanda na wote tumeshuhudia Juhudi za Mheshimiwa Rais za Kutafuta wawekezaji kutoka Mataifa mbalimbali duniani ili yawekeze nchini.

Ndugu zangu yako Mengi sana aliyofanya Rais Magufuli  mwenye macho haambiwi tazama ila naomba niishie hapo.  Ijapokuwa Bado Changamoto ni nyingi na watu wataona Maisha yamekuwa magumu lakini tutambue na kuelewa hali hiyo haina budi kuja kwani  Nchi iko katika kipindi cha Mabadiriko ya kiuchumi kitaalamu tunaita " TRANSITION PERIOD " ambapo kutokana na Juhudi za Mheshimiwa Rais kuujenga uchumi wa Nchi yetu ni lazima mwanzoni tutaona Mabadiriko fulani fulani hivyo Watanzania wenzangu tuvute subira kwa maisha Mazuri yaja. Tumpe nafasi Mh. Rais apambane kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi yetu na sisi kwa nafasi zetu tumpe ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kazi kwa Bidii sana.

Ama Kwa Hakika Rais wetu anastahili pongezi nyingi sana na Mimi Robert PJN Kaseko Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha nichukue nafasi hii kukupongeza Rais wangu na Mwenyekiti wangu CCM Taifa Mh. DKT. John Pombe Magufuli kwa kutuletea Maendeleo makubwa na Mabadiriko ya kweli kwa kipindi cha Mwaka mmoja tunashirikiana toka tukuchague utuongoze, Mabadiriko  ambayo kiukweli sisi Wananchi wa Tanzania tulisubiri kwa Muda mrefu sana na nizidi kukutia moyo Mh. Rais usirudi nyuma endelea mbele tunatambua vikwazo ni vingi na Kazi ni ngumu lakini namuomba Mwenyezi Mungu azidi kukutia nguvu, akupe afya njema na ulinzi wake ili uendelee vyema kuwaletea Maendeleo Wananchi wako maana wewe ni Mchapa Kazi Kwelikweli tunakufahamu vizuri. HAPA KAZI TU. CCM Hoyeeeeeee.

Robert PJN Kaseko
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha
November 04, 2016.

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger