Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ahmed Msangi alisema jana kuwa uporaji huo umefanyika Desemba 4, mwaka huu 6.02 usiku katika Mtaa wa Igogo Wilaya ya Nyamagana.
Kamanda Msangi alisema mlinzi huyo aliporwa bunduki hiyo iliyokuwa na risasi sita baada ya kuvamiwa na watu wawili akiwa kwenye lindo lake.
“Mlinzi huyo alikuwa kwenye lindo la ghala la RTC lililokodiwa na Kampuni ya Mohamed Enterprises linalohifadhi bidhaa mbalimbali za chakula,” alieleza Msangi.
“Alivamiwa na watu wawili ambao hakuwafahamu ambao walimpiga na kitu kizito kichwani na kupoteza fahamu na kupora bunduki hiyo ikiwa na risasi sita kwenye magazini yake,” alisema Msangi na kuongeza kuwa kuporwa bunduki kwa mlinzi huyo, alizembea na watu hao wakapata upenyo wa kufanya uhalifu wa kuipora bunduki hiyo.
Alisema Polisi inawashikilia watu wawili wanaodaiwa kuhusika kwenye tukio hilo na kwamba upelelezi na msako mkali wa kuitafuta silaha hiyo unaendelea.
“Mlinzi aliyejeruhiwa amepatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri,” alifafanua na kutoa mwito kwa wakazi wa Jiji na Mkoa wa Mwanza watakaopata taarifa za ilipofichwa bunduki hiyo kabla haijaleta madhara kwa wananchi.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment