Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dk Khatibu Kazungu alisema kwa mara ya kwanza meli kubwa ijulikanayo Morning Composer imetia nanga na kushusha malori 651 katika bandari hiyo.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya magari hayo bandarini hapo jana, Dk Kazungu alisema kufika kwa meli hiyo kutoka mashariki ya mbali kumefungua fursa za kiuchumi Mtwara na kuitangazia dunia kwamba bandari hiyo ina uwezo kama zilivyo nyingine duniani.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment