Wakichangia hotuba ya Rais Magufuli, iliyosomwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao cha tano cha bunge hilo,kilichofanyika Machi 8 mwaka huu, jijini Dar es salaam, wabunge hao walisema vita dhidi yaRRushwa inayofanywa na Rais Magufuli iguse pia jumuiya hiyo.
Mbunge Mike Sebalu kutoka Uganda, alisema Rais Magufuli tangu amechaguliwa amejitahidi kufanya mambo makubwa kwa taifa la Tanzania ikiwamo vita dhidi ya rushwa na kurejesha uwajibikaji katika serikali yake.
Hata hivyo, aliwaomba wabunge wa Tanzania, kuliwezesha EALA kukutana na Magufuli, ili kujadiliana mwenendo wa jumuiya hiyo.
Mbunge Shyrose Bhanji wa Tanzania, alisema kasi ya Rais Magufuli, imekuwa na manufaa makubwa sio kwa watanzania bali kwa wananchi wote wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
"vita dhidi ya rushwa na ufisadi ambayo imeanzishwa na Rais Magufuli, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, inapaswa kuungwa mkono na bunge hilo"alisema
Mbunge Martin Ngoga wa Rwanda, alisema kasi ya Rais Magufuli ambaye ni mwenyekitiwa jumuiya hiyo,inapaswa kuungwa mkono na sio vibaya jumuiya ya Afrika ya Mashariki, kuonesha kwa dhati inapambana na rushwa.
"Rais Magufuli anafanyakazi nzuri sana na sisi kama wabunge tunamuuunga mkono ili kuwa na manufaa katika jumuiya ya Afrika ya Mashariki mataifa yote yanapaswa kushirikiana kuondoa rushwa"alisema.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment