Oct 20, 2016

ZITTO Kabwe: Muswada wa Huduma za Habari(Media Services Bill 2016) ni HATARI

Serikali ya awamu ya Tano imewasilisha Bungeni Muswada wa Sheria kutunga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari.

Muswada wa Sheria hiyo sasa upo mbele ya kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kuchambuliwa na kisha kuwasilishwa Bungeni. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kanuni ya 84 Kamati ya Bunge inawajibika kuutangaza muswada na kupokea maoni ya wadau mbali mbali. Kwa hakika wadau wa muswada huu ni wananchi wote kwani haki ya kupata habari ni haki ya kikatiba.

Hata hivyo, waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari na mitambo ya kuchapisha magazeti na majarida ni makundi yatakayoathirika moja kwa moja na muswada huu utakapokuwa sheria. Hata hivyo, muswada unapelekwa mbio na mwenyekiti wa Kamati katishia kuwa iwapo wadau hawatatoa maoni, Kamati yake itaendelea na kazi zake za kutunga sheria.

Kwa muda mrefu sana Waandishi wa habari na wanazuoni mbalimbali wamekuwa wakitaka kuwepo na sheria ya kusimamia tasnia ya habari. Ninaambiwa kuwa juhudi za kutunga sheria hii ni mchakato wa zaidi ya miaka 20, tangu mwaka 1993 ambapo muswada wa kusajili waandishi wa habari uliondolewa Bungeni baada ya kuwasilishwa na Dr. William Shija wakati ule akiwa Waziri wa Wizara ya Habari na Utangazaji, ambaye sasa ni marehemu.

Vile vile kumekuwa na kilio kikubwa cha vyombo vya habari kufungiwa kwa kutumia Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo inampa mamlaka makubwa sana waziri wa Habari. Wananchi wengi na wapenda demokrasia walitaraji kwamba sheria mpya ingeweza kuondoa sheria kandamizi na kuweka uhuru wa vyombo vya habari ipasavyo. Hicho sicho kilicholetwa na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli.

Muswada uliopo mbele ya kamati ya Bunge unatoa tafsiri pana sana ya vyombo vya habari. Sehemu ya 3 ya Muswada inatamka chombo cha habari ni pamoja na gazeti, kituo cha radio na televisheni ikiwemo mitandao ya kijamii (online platforms). Muswada unatamka kuwa ni lazima ‘media house’ iwe na leseni maalumu kwa ajili kufanya kazi na waandishi wa chombo hicho ni lazima waandikishwe kwenye chombo kiitwacho Accreditation Board (Bodi ya Ithibati).

Iwapo sheria hii itatungwa, maana yake ni kwamba mtandao kama wa JamiiForums utapaswa kuandikishwa na watu wote wanaotoa maoni yao kwenye mtandao huo lazima wawe na ithibati! Haitaishia hapo, bali hata blogs nk zitapaswa kuandikishwa kama ilivyo magazeti.

Hatua hii itaminya sana uhuru wa watu kupata habari na kupashana habari. Hata uhuru wa kujieleza utaminywa sana kupitia mitandao ya kijamii.

Muswada unataka kuwepo na sheria ya Serikali kuamua vyombo vya habari viandike nini na vitanagze nini. Sehemu ya 7(1)(b)(iv) inatamka wazi kwamba Waziri anaweza kuagiza chombo chochote cha habari cha binafsi kutangaza habari Fulani au masuala Fulani yenye umuhimu kwa Taifa.

Itakumbukwa kwamba muswada uliopita ambao ulikataliwa ulitaka ifikapo saa mbili usiku televisheni na radio zote ziungane na TBC kutangaza taarifa ya habari. Kifungu hiki ndio kitatumika kufanya suala hilo kwa amri ya Waziri.

Kifungu hiki pia kinampa Waziri wa Habari mamlaka ya kuelekeza chombo cha habari kutotoa habari Fulani kwa utashi wa Waziri. Ni dhahiri kuwa huu ni ukiukwaji mkubwa sana wa uhuru wa habari na kuwa kikwazo kikubwa kwa kazi za waandishi. Kwa kutumia kifungu hiki Waziri wa Habari anaweza kuagiza magazeti yote yasiandike habari za IPTL Tegeta Escrow na Waziri atakuwa ndani ya sheria.

Muswada pia unampa Waziri wa Habari mamlaka ya kutoa Masharti ya Kazi za vyombo vya habari ( Terms and Conditions ). Hii inatia nguvu kifungu hicho hapo juu kuhusu maelekezo ya habari za kutolewa na kutotolewa na vyombo vya habari.

Muswada huu umerudisha vifungu vyote kandamizi vilivyopo kwenye sheria ya magazeti ya mwaka 1976. Kwa mfano kifungu cha 54-56 kinampa Waziri haki ya kutamka kwamba gazeti Fulani au kitabu Fulani kisisambazwe nchini au kuzalishwa nchini.

Kwenye masuala mengine, Mkurugenzi wa Habari Maelezo na Jeshi la Polisi linaweza kuingia kwa nguvu na kuchukua mitambo inayozalisha magazeti kwa sababu tu gazeti hilo limechapisha habari ambayo kwa maoni ya Serikali ni habari za kichochezi.

Muswada umetafsiri uchochezi kuwa ni pamoja na kuandika au kutangaza mambo ambayo yanaweza kutafsiriwa kuwa yanaleta chuki ya wananchi dhidi ya Serikali. Kwa kutumia kifungu hiki, mbunge wa upinzani akihutubia na kuonyesha ufisadi Serikalini, sheria hii inaweza kutumika kufuta vyombo vya habari vilivyoandika au kutangaza habari hiyo.

Kwa ufupi, huu ni muswada mbaya kuliko sheria ya magazeti ya sasa. Huu muswada unairudisha nchi nyuma katika juhudi za kujenga Taifa lenye Haki na wajibu. Ni sheria kandamizi ambazo kama Jaji Francis Nyalali angekuwa hai angeijumuisha katika sheria 40 kandamizi.

Serikali ya awamu ya Tano imeamua kujenga Taifa lenye giza. Rais Magufuli ameamua kukataa kata kata kuhojiwa na kukosolewa kwa kuhakikisha kuwa anavibana vyombo vya habari nchini.

Nilipata kusema huko nyuma kwamba, Serikali ikishamaliza kuvibana vyama vya upinzani itavibana vyombo vya habari. Utabiri ule umetimia kupitia sheria ya huduma za habari inayoelekea kutungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dodoma, 20/10/2016

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Soma Hizi Habari Zetu Kirahisi Kupitia Application ya Simu ya Udaku Special, Bonyeza HAPA
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 [disqus]:

Post a Comment

Follow Us

Popular Posts

Powered by Blogger.

MKRdezign

Blog Archive

Technology

[blogger]
Contact us
Ajirayako.co.tz
E-mail: ajirayako@gmail.com
DISCLAIMER:
This Website |Ajirayako.co.tz| is Not Affiliated In Any Way
With The Companies Whose Vacancies Are Published Here.
AVOID SCAMS
Never Pay to Have Your CV/Application Pushed Forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a scam.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tags

Abdallah Zombe (3) ACT Wazalendo (7) Afande Sele (6) Afya (42) Air Tanzania (11) Ajali (31) Ajira (16) Akson Tulia (4) Alberto Msando (1) Ali Kiba (10) Almaz Ayana (1) Anna Makinda (2) Anthony Lusekelo (1) Arusha (1) Arusha Felix Ntibenda (1) Asha Rose Migiro (2) Askofu Gwajima (6) ATCL (3) Augustine Lyatonga Mrema (4) Aunty Ezekiel (2) Babu Tale (2) Bajeti (1) Bakwata (3) Baletol (1) Bandari (3) Baraka da Prince (2) Bavicha (1) Benjamin Mkapa (1) Benki Kuu Tanzania (1) Bernad Membe (1) Biashara (1) Bodi ya Mikopo (1) Bongo Movies (7) BOT (1) Breaking News (3) Buhari (1) Bungeni (48) Burudani (45) CCM (5) Chadema (20) Charles Kitwanga (3) Chibok (1) Chid Benz (2) Chris Brown (3) Clouds FM (1) CUF (26) Dangote (3) Daniel Ole Njolay (1) Dart (2) David Kafulila (7) Desmond Tutu (2) Diamond Platnumz (18) DJ Fetty (1) Dk. Reginald Mengi (1) Donald Trump (23) Dr Mwaka (1) Dr Mwaka Aacha Vilio Kwa Wagonjwa...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30 (1) DR Shein (2) Dr Slaa (4) Dr. Ramadhan Kitwana Dau (1) Edo Kumwembe (1) Edward Lowassa (30) Elimu (75) EPA (1) Escrow (3) Ester Bulaya (9) Faiza Ally (1) Fast Jet (1) Featured (3) Flaviana Matata (1) Freeman Mbowe (31) Fumanizi (1) Gadner (1) George Masaju Masaju (1) Gerald Hando (1) Godbless Lema (31) Godwin Gondwe (1) Halima Mdee (2) Hamad Rashid (1) Harmonize (3) Hillary Clinton (3) Iddi Amini Dadaa (1) Idriss Sultan (2) Iphone (1) Irene Uwoya (1) Ivo Mapunda (1) Jack Wolper (3) Jaji Francis Mutungi (3) Jakaya Kikwete (13) Jambazi (2) James Mbatia (1) January Makamba (1) JB (1) Jecha Salim (1) Jenerali Ulimwengu (1) Jerry Muro (3) Jeshi la Polisi (32) Jobs (1) John Cheyo (1) John Mnyika (3) John Pombe Magufuli (83) Joseph Kabila (2) Josephine Mshumbushi (1) Joshua Nassari (1) Julieth Kairuki (1) Julius Mtatiro (9) Jussa (1) Kamanda Sirro (1) Kenyan News (14) KFC (1) Kicheko (1) Kigwangalla (1) Kilimo (1) Kinana (3) Kitanzi (1) Koffi Olomide (2) Korea (1) Kuliko Jana (1) Leicester City (1) Livingstone Lusinde (1) Lugumi (1) Lulu Michael (1) Maajabu (3) Maalim Seif (14) Madam Rita (1) Madawa ya Kulevya (7) Magazeti (49) Mahakamani (7) Mai Mai (4) Maisha (2) Majambazi (7) Makahaba (1) Makalio Makubwa (1) Makamba (1) Malaika (1) Malezi (1) Mama Salma (1) Man Fongo (2) Man United (1) Mange Kimambi (2) Manji (7) mape (1) Mapenzi (76) Marcus Rashford (1) Mashine ya MRI (1) Matiko (1) Matokeo (3) Mauaji (31) Mauji (2) Mbeya (2) Mbunge Lusinde (1) Mbwana Samatta (8) Mchungaji Anthony Lusekelo (1) Meya wa Kinondoni (1) Michael Shirima (1) Michez (1) Michezo (201) Miss Tanzania (2) Mizengo Pinda (1) Mongela (1) Mr Blue (3) Mrema (7) Mrisho Gambo (3) Mrisho Mpoto (2) Msigwa (2) Mugabe (1) Museven (1) Music (85) Muungano (1) Mwakyembe (2) Mwanafunzi (3) Mwendokasi (1) Mwigulu Nchemba (2) Nape Nnauye (13) Navy Kenzo (1) Nay wa Mitego (2) Ndanda FC (1) Ndugai (1) Necta (3) Nida (1) Nigeria (2) NSSF (1) Nuh Mziwanda (2) Nyerere (1) Obama (9) Ommy Dimpoz (2) Original Comedy (2) Oscar Pistorius (1) Paul Makonda (34) Paul Pogba (2) Pep Guardiola (1) Peter Msigwa (4) Petitman (1) Polisi (4) Pombe (1) Pride (1) Prof Mkumbo (2) Prof. Benno Ndulu (1) Prof. Ibrahim Lipumba (12) Prof. Lipumba (23) Prof. Tibaijuka (3) Profesa Benno Ndulu. (1) Profesa Muhongo (3) Q-Chief (1) Raila Odinga (2) Rais Magufuli (35) Ray C (1) Reginald Mengi (2) Rihanna (1) Robert Mugabe (4) Ruby (5) Rushwa (3) Sadaka (1) Saed Kubenea (3) Saida Karoli (2) Salama Jabir (1) Salum Mwalimu (2) Samia Suluhu (1) Samsung Galaxy (1) Samwel Sitta (5) Sauti Sol (1) SBL (1) Scorpion (3) Serengeti Boys (1) Shamsa Ford (2) Sheikh Abubakar Zubeiry (2) Shibuda (2) Shilole (1) Siasa (1945) Siasa Huru App (3) Siasa za Kenya (1) Simba (1) Slaa (1) Snura (1) South Africa (1) Sudan (1) Sugu (1) Sukari (4) Sumaye (8) Supu ya Pweza (1) Tanesco (9) Tanzia (22) TB Joshua (4) TBS (1) TCRA (5) TCU (4) Technology (3) Tetemeko (13) TFDA (1) Thereza May (1) Thomas Mashali (1) TRA (4) Tundu Lisu (20) Tyrant (1) Ubakaji (4) Uchambuzi (1) Uchawi (1) Uchumi (90) Udaku (46) Udaku Spesho (21) UDSM (1) Ufisadi (2) Ugaidi (6) Uhuru Kenyatta (2) Ujambazi (4) Ujauzito (1) Ukahaba (1) Ukatili (1) Ukawa (11) Ukuta (11) Ummy Mwalimu (1) Urembo (15) Ushirikina (1) Utafiti (2) Utapeli (3) UVCCM (4) Vioja (1) Wastara (1) Watumishi Hewa (1) Waziri Mahiga (2) Waziri Mkuu Majaliwa (18) Wema Sepetu (6) Wiliam Lukuvi (6) Yanga (7) Yaya Toure (1) Zitto Kabwe (33) Zuckerberg Mark (1)

Categories

Advertisement

Main Ad

Facebook

Responsive Ads Here

Featured

Recent

Udaku Special Test

Copyright © Udaku Special Test | Powered by Blogger