Waziri Jafo amepiga marufuku hayo mjini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya sheria mpya ya manunuzi kwa maafisa manunuzi mjini humo.
“Wakandarasi wengine wanapata tenda ya mabilioni ya fedha lakini hata ofisi maalum hawana, na bodi za manunuzi zimefanya na kumpitisha mtu ambaye hata ofisi ambayo inasema hii conduct person inapatikana sehemu fulani lakini watu hata ofisi hawana. Na wengine wana panga katika ofisi za ubabaishaji na hili ni jukumu letu sisi bodi ya manunuzi,” alisema Jafo.
“Watu wote watakaopatikana katika manunuzi ya serikali yetu waweze kuwa ni watu makini ambao mwisho wa siku tunapata ile kitu inayoitwa value of money. Ndugu zangu katika kupitisha sheria ya manunuzi mwaka huu matokeo yake ni kwamba kumelenga kuokoa fedha kubwa sana na fedha nyingi sana za wananchi,” aliongeza.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment