Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond Platnumz aliandika “mapema Leo ofisini kwangu, tukijadili Mawili matatu kuhusu namna ya Kuipeleka sanaa yetu kileleni na Mh: Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mh: Nape Nauye….. Shukran sana Mkuu kwa kuendelea kutujali Wasanii, it was a great Meeting🙏”
Adhia, baadhi ya mambo ambayo Diamond pamoja uongozi wake walijadiliana na Waziri Nnauye ni pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili kama kupunjwa mapato yatokanayo na miito ya simu (Caller tunes), wizi wa kazi za wasanii, kupata eneo (Ukumbi wa Kisasa) kwa ajili ya kufanyia maonesho makubwa ya muziki, wasanii kupata elimu juu ya kulipa kodi kwa kazi zao na kuongeza kiwango cha uwiano kwa nyimbo za kitanzania zinazopigwa redioni dhidi ya nyimbo za kigeni.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment