Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo ni kati ya watano waliokamatwa kwa tuhuma za kuvamia maduka makubwa na kupora mali jijini Dar es Salaam.
Sirro alisema tukio hilo lilitokea Septemba 14 eneo la Ununio wakati mtuhumiwa akiwapeleka polisi kuwaonyesha ilipokuwa imefichwa silaha kwenye majaruba ya chumvi.
Alisema mtuhumiwa alifariki dunia wakati akipelekwa hospitali kwa matibabu kutokana na kutokwa damu nyingi.
Awali, alisema watuhumiwa hao, akiwamo mwanamke, walikamatwa katika eneo la Goba na baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika na matukio hayo.
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment