Kiasi hicho cha fedha kimetokana na ahadi na michango ya fedha za taslim baada ya wadau mbalimbali kuitikia wito wa matembezi hayo yaliyoitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ili kuwachangia wananchi hao waliothiriwa vibaya na tetemeko hilo.
Matembezi hayo ya kilomita tano yameanzia na kumalizikia katika eneo la ufukwe wa Coco jijini hapa na kuongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.
Katika matembezi mengine ya kuwachangia wananchi hao yaliyofanyika katikati ya jiji, Chama cha madalali wa huduma za bima (Tiba) kimetoa hundi ya Sh20 kwa ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuchangia waathirika wa tetemeko hilo lililogharimu maisha ya watu 19 mpaka sasa.
Rais wa Tiba, Mohamed Jaffer amesema kilichotokea Kagera kinapaswa kuwa fundisho kwa watu kuwa na utaratibu wa kukata bima zikiwemo zenye sera ya kuhudumia walioathiriwa na majanga.
Habari zaidi kukujia ndani ya gazeti la Mwananchi kesho na kwenye epaper
Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
0 [disqus]:
Post a Comment